Raila aiomba Marekani kumaliza mkwamo wa kisiasa Kenya

Kingfisher

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2015
Posts
4,740
Reaction score
7,679
Juhudi za wajumbe wenu hazijafanikiwa mpaka sasa kuzima mgogoro na hebu niseme wazi Kwa namna Fulani wamechangia katika mgogoro huu.

Ina maana kwamba EAC na hata AU wameshindwa kutatua mgogoro huu mpaka Odinga (raisi wa mioyo ya baadhi ya wakenya) akaombe support kwa Trump?


..........................................................


Nairobi, Kenya. Kiongozi wa muungano wa Nasa Raila Odinga jana aliwaomba washirika wa maendeleo wa kimataifa wa Kenya kujihusisha kikamilifu kusaidia kumaliza mkwamo wa kisiasa nchini.

Katika hotuba yake ya dakika 30 akiwa jijini Washington, DC, Marekani Odinga amezitaka nchi za Magharibi kuchukua hatua akisema wanadiplomasia wan chi hizo wamejikita zaidi kukabiliana na kukua kwa siasa kali na ugaidi huku wakipuuza ufinyu wa demokrasia katika mgogoro juu ya uchaguzi wa rais mwaka huu.

“Nimekuja huku Washington kuwaletea ujumbe rahisi: Tunahitaji mshiriki kwa nguvu na kutumia mikono mingi iliyonayo serikali yenu ili kuwasaidia wajumbe wenu walioko Nairobi,” alisema katika Kituo cha Usalama na Mafunzo ya Kimataifa.

“Juhudi za wajumbe wenu hazijafanikiwa mpaka sasa kuzima mgogoro na hebu niseme wazi: Kwa namna Fulani wamechangia katika mgogoro huu,” alisema na akazishutumu nchi za magharibi kwa kuiacha Kenya ielekea njia ya utawala wa mtu mmoja na udikteta.

“Mgogoro wa sasa wa Kenya kuhusu uchaguzi haujachochewa na wizi wa wazi wa kura kwa mara ya tatu pekee...Hebu niweke sawa: Kenya inapiga hatua kuelekea kuwa nchi ya kidikteta,” alisema.

“Serikali ya Jubilee imepora mamlaka ya kila taasisi ili kufanikisha lengo la kulidhibiti taifa au walivyojitangazia kutawala hadi mwaka 2032,” alisema Odinga na akaongeza kwamba anaamini Kenya inahitaji uchaguzi mpya na wa kuaminika.
Source: MCL
 
EAC and AU all are bogus! 99.9999% EAC and AU are dictators, 0.1111111% hawezi kukbali 99.99999% imsuluhishe!
 
Kwa namna siasa za bara la Africa zilivyo Odinga ndiyo basi tena. Atakuwa kama maalim Seif wa Zanzibar.
 
unataka vipi urais wakati hata hukushiriki uchaguzi..eti jubilee ni madikteta!!
hivi hajui kuwa rafiki yake ndio dikteta hatari sana?
 
Kakwepa kuchaguliwa kwa kula ambayo ndiyo demokrasia(wengi wape) sababu anajua hawezi shinda.
Kakimbilia kukwamisha free election ili apate visingizio vya kulazimisha serikali ya umoja wa kitaifa au nusu mkate kama wakenya wanavyosema.
Kama kuna mtu ambaye ni undemocratic, chaotic, tyranny, power monger ni RAO, Nashangaa sana kwamba bado ana wafuasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…