Raila Amolo Odinga: Kioo cha haki na mfano wa kiongozi bora.

herikipaji

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2016
Posts
1,198
Reaction score
1,369
Nampongeza sana Raila Odinga na muungano wa NASA kwa ushindi waliopata hii leo kwa mahakama kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi uliompa ushindi wa urais.

Nawapomgeza pia majaji walioendesha kesi hii ya kihistoria si tu Afrika pia duniani kwa ujumla kwa kusimamia haki na tumejifunza sana.

Nawapongeza wakenya wote wanaojielewa kwa kupigania haki zao za kiraia na kutokubali dhulma na uonevu.

Ni ushindi mukubwa sana kwa wapenda haki si tu wakenya lakini kwa wote wa mataifa mbalimbali duniani Mwanaharakati Dr. Martin L. King Jr. aliwahi kusema nanukuu- “Injustice anywhere is a threat to justice everywhere.
Haki kutendeka kwa wakenya ni furaha kwa wote wapenda haki.

Baadhi ya watanzania walimbeza sana Raila Odinga na NASA nafikiri kwa kutokua na uelewa tu mzuri wa mambo ya siasa-geopolitics hawa siyo kosa lao tatizo tu ni upofu wa fikra kwani kuna kundi kubwa la watanzania ambao hawajitambui wao ni bendera fuata upepo hasa vijana.
Sasa wanapongeza demokrasia ya Kenya, lakini hawaoni harakati za kiongozi Raila Odinga za kufa na kupona kwa kuipigania hiyo demokrasia na haki kwa wakenya, hili hawa watu hawalioni au tu wanajitia upofu kama kawaida yao.

IEBC iundwe upya watafutwe watu wataosimamia haki bila upendeleo kwa mgombea yeyote yule sasa ili kusimamia huo uchaguzi utaofata na hawa wa sasa ni vema waadhibiwe iwe funzo kwa wengine wenye kupenda dhulma.

Natumai sasa NASA watashinda kama uchaguzi utakuwa huru na haki na rais atakuwa Raila Odinga, sifa zote za uongozi bora huyu anazo na ni mpenda haki, na anapendwa sana Kenya.
Raila ni kiongozi halisi sababu amepigania katiba mpya na watawala kuheshimu na kufata hiyo katiba hakuogopa mabomu wala virungu vya mapolisi, amepigania utawala wa sheria hivyo anastahili heshima.

MODS naombeni sana msiunganishe hii mada sababu ina ujumbe tofauti.
 
Nakuunga mkono 100% ila nashindwa kufikiria kuhusu wale waangalizi wa kimataifa iwapo wanaweza
wakakubaliana na wewe...................
 
Nakuunga mkono 100% ila nashindwa kufikiria kuhusu wale waangalizi wa kimataifa iwapo wanaweza
wakakubaliana na wewe...................
Ndugu hili ni pigo kwa wale wanaojiita waangalizi wa kimataifa, inaonekana wale watu hawapo kwa maslahi ya raia wa taifa husika linalofanya uchaguzi ila wapo kwa ajili ya maslahi yao tu na hata hawaangalii kama haki imetendeka au ni dhulma tupu katika uchaguzi husika.
Ni wa kupuuzwa tu hao tena aibu hii sijui wataibebea wapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…