Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Siasa za kiafrika ni za kipekee sana. Hazifanani na siasa za mabara mengine. Zimejaa mambo mengi ya chini kwa chini.
Raila Amolo Odinga anahamasisha maandamano miongoni mwa wafuasi wake halafu yeye anapanda ndege na kwenda zake ughaibuni.
Yeye huko nje anapo pa kufikia, anapo pa kuishi. Wale ndugu zangu na mimi wanaoishi kwenye mbavu za mbwa, wasio na passport wasio na pa kukimbilia, ndio wanaokutana na maumivu ya virungu na risasi za polisi!!.
Siasa za kishabiki haziwaachi wananchi wa kawaida, salama. Ni wao wanaotolewa "sadaka" kwenye michakato ya kisiasa, na ni kwa faida ya malengo na ndoto za kisiasa za wachache.
Hati za kusafiria za wanasiasa wa kiafrika zinapokuwa zimejaa basi hata lile zoezi la kupata nyingine hufanyika chapchap, na huko nje wanapo mahali pa kujihifadhi. Taabu inabakia kwa waungwana wanaochoma matairi barabarani wakitegemea TZ 11 ndio iwaokoe wakati polisi wanapoanzisha vichapo.
Hizi ndizo siasa za kiafrika. Politics made in Africa. Wapambe ambao wanayo maisha angalau yenye kueleweka na wao huwa na hati za kusafiri lakini huko nje hakuna anayewajua.