Raila anahamasisha maandamano halafu yeye huyooo anapanda ndege.

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
18,487
Reaction score
13,611
Siasa za kiafrika ni za kipekee sana. Hazifanani na siasa za mabara mengine. Zimejaa mambo mengi ya chini kwa chini.

Raila Amolo Odinga anahamasisha maandamano miongoni mwa wafuasi wake halafu yeye anapanda ndege na kwenda zake ughaibuni.

Yeye huko nje anapo pa kufikia, anapo pa kuishi. Wale ndugu zangu na mimi wanaoishi kwenye mbavu za mbwa, wasio na passport wasio na pa kukimbilia, ndio wanaokutana na maumivu ya virungu na risasi za polisi!!.

Siasa za kishabiki haziwaachi wananchi wa kawaida, salama. Ni wao wanaotolewa "sadaka" kwenye michakato ya kisiasa, na ni kwa faida ya malengo na ndoto za kisiasa za wachache.

Hati za kusafiria za wanasiasa wa kiafrika zinapokuwa zimejaa basi hata lile zoezi la kupata nyingine hufanyika chapchap, na huko nje wanapo mahali pa kujihifadhi. Taabu inabakia kwa waungwana wanaochoma matairi barabarani wakitegemea TZ 11 ndio iwaokoe wakati polisi wanapoanzisha vichapo.

Hizi ndizo siasa za kiafrika. Politics made in Africa. Wapambe ambao wanayo maisha angalau yenye kueleweka na wao huwa na hati za kusafiri lakini huko nje hakuna anayewajua.
 
Olye mutwishi yawe omyame
 
Ndo Maana mbowe alihairisha ukuta kwa kisingizio cha ushauri
 
Inasikitisha sana mkuu.
Leo jioni nikiwa naangalia CITIZEN TV habari ya saa 1 usiku, niliumia sana kumuona binti mdogo wa miaka 2 akiwa hospitali na jeraha la kupigwa risasi begani huko Kisumu,Kenya. Niliumia sana sana kupita maelezo. Nikijiuliza maswali mengi bila kupata majibu.
 
Wakati mwingine mwanasiasa ni kama mwanaume mtongozaji, akishapata akitakacho anaendelea na maisha yake.
 
Phillipo Bukililo,

..hata "mzee kipara" akisema "nita deal nao" huwa hajitokezi kukabiliana na hao mahasimu wake bali hutuma watu fulani wenye bunduki na mabomu ya machozi.
 

..Tz wakati yalipotupwa mabomu kwenye mkutano wa Chadema Arusha kuna mtoto alipoteza maisha.

..umesahau mwandishi Daudi Mwangosi alivyouawa kwa bomu la Polisi ambapo mwili wake ulisambaratishwa ukawa kama nyama ya kusaga?

..Tunaweza kusikitika kwa yanayotokea Kenya lakini Tanzania nako hali siyo nzuri.
 
Jikite kwenye mada. Mada hapa inamzungumzia RAO na hali ya kisiasa nchini Kenya kwa sasa. Hayo uliyoandika yalishapita na tulilaani na kusikitika kama Watanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…