Raila anapanga 'kuapishwa' Tanzania

SNAP J

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2013
Posts
7,106
Reaction score
8,043
WABUNGE wa Chama cha Jubilee wamedai kinara wa muungano mkuu wa upinzani wa NASA, Raila Odinga, anashirikiana na mataifa ya kigeni kula njama za kujitangaza mshindi wa uchaguzi wa urais na kwenda kuapishwa nchini Tanzania.

Hayo ni kwa mujibu wa wabunge watatu wa chama hicho na majimbo yao kwenye mabano, Muthomi Njuki (Chuka/lgambangombe), Moses Kuria (Gatundu Kusini ) Kimani Ichungwa (Kikuyu) na Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Tharaka Nithi, Beatrice Nkatha.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Chuka, Kaunti ya Tharaka Nithi, wabunge hao walisema lengo la Raila kutaka muungano wa NASA kuwa na kituo cha kuhesabu kura ni kujitangaza mshindi kisha aende kuapishwa katika nchi jirani ya Tanzania.

Walionya hatua hiyo itazua ghasia baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 8 kama ilivyotokea baada ya uchaguzi mkuu wa 2007.

Viongozi wa Jubilee wamekuwa wakipinga azma ya NASA kuwa na kituo cha kuhesabu kura wakisema ni Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) pekee inayoruhusiwa kisheria kuhesabu na kutangaza matokeo.

“Tunajua Odinga anapanga kujitangaza mshindi na kwenda kujiapisha Tanzania akishindwa kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 8,” alisema Icungwa.

Alisema kujitangazia matokeo ya uchaguzi mkuu ni sawa na uhaini kwa sababu hilo ni jukumu la IEBC pekee kufanya hivyo.

Njuki alidai ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 zilisababishwa na kukataa matokeo ya uchaguzi mkuu kulikofanywa na Odinga.

Kuria alisema Odinga anahisi kushindwa na hivyo anatafuta njia za kupinga matokeo.

Chanzo: Gazeti Mtanzania.
 
Nadhani ndio maana Chato kunajengwa uwanja wa ndege ili isiwe tabu Raila akiongoza Kenya kwenye ikulu ndogo ya swahiba wake
 
Halafu na lile king'ang'anizi na mbishi balaa
 
Huyo Odinga aache upuuzi wake kumbe ndiyo maana Chato International Airport inajengwa haraka-haraka.
 
Shenzy kabisa ukouko kwao sisi hatutaki hizo mambo aisee
 
10 RICHEST families in
KENYA
1. Moi Family
2. Nicholas Biwott
3. Kenyatta family
4. Joshua Kulei
5. Njenga Karume
6. Philip Ndegwa family
7. Odinga family
8. Manu Chandaria
9. S. K Macharia
10. Mwai Kibaki
Did you see my family or
your family name
anywhere on the list???NO!
I don't think so! Alafu
wewe ndio utakua
umebeba ile panga kubwa
kabisa after 8th
August unataka kunichinja
na tuko class
moja! Mimi sina place
ingine naweza
torokea ,so pliz, let us
remain peaceful
after elections, Raila
Odinga
na Uhuru Kenyatta
hakujui wala hawanijui, wao
watakua wame-relax
kwao wamezungukwa na
GSU...wewe na mimi hatuna GSU!!!!
MY POINT IS PEACE NO MATTER WOT!!!!!
[HASHTAG]#share[/HASHTAG] widely tusipigane bure!!![emoji106]
 
Ujumbe mwanana huu, usambazwe kwenye blogs zao.
 

Hahaha Nimeipenda koment hii
safi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…