Raila na NASA wapinga ushindi wa Uhuru Kenyatta Mahakamani

Raila na NASA wapinga ushindi wa Uhuru Kenyatta Mahakamani

pantheraleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
692
Reaction score
880
Muungano wa Upinzani, NASA umefungua kesi usiku huu kwenye Mahakama Kuu kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika Uchaguzi Mkuu.
20953298_1969087483327736_5915454083103947175_n.jpg

Muungano wa upinzani nchini Kenya, NASA, Ijumaa usiku umewasilisha malalamiko kwenye mahakama ya juu, kupinga uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta uliotangazwa wiki moja iliyopita na tume ya uchaguzi na mipaka, IEBC.

Mawakili wa muungano huo waliwasilisha nyaraka zao katika mahakama ya juu mjini Nairobi saa tatu na nusu za usiku.

Hatua hiyo ilikuwa imesubiriwa na wafuasi wengi wa muungano huo, baada ya aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya NASA, Raila Odinga, kutangaza siku ya Jumatano kwamba wangewasilisha hoja yao mahakamani.

Raila na wenzake kwenye muungano huo wanashikilia kwamba uchaguzi wa mwaka huu uligubikwa na dosari na kwamba yeye ndiye aliyestahiki kutangazwa mshindi.

Kwa mujibu wa katiba ya Kenya, mahakama ya juu inazo siku 14 za kusikiliza na kuamua kesi hiyo.

Kufuatia uchaguzi uliofanyika siku ya Jumanne tarehe 8 mwezi Agosti, IEBC ilitangaza kwamba Kenyatta alishinda kwa kura 8,203,290 huku Raila Odinga akipata 6,762,224.

Odinga amesema kuwa ushindi huo wa Uhuru si halali na kwamba ulikarabatiwa na kompyuta.

Jaji mkuu wa Kenya David Maraga, amesema kwamba mahakama ya juu iko tayari kufanya kazi usiku na hata wikendi ili kusikiliza na kuamua kesi hiyo katika muda uliowekwa kikatiba.

Kuapishwa kwa rais ambako kulikuwa kumepangwa sasa kumeahirishwa hadi pale mahakama itakapotoa uamuzi wake.

https://www.voaswahili.com/a/raila-awasilisha-kesi-mahakamani/3991686.html
 
Sasa vile NASA ilishindwa kwa maGavana,MP's na Seneta wengi hio pia ni udanganyifu? RAO has too much pride and big ego to accept defeat .Huyu jamaa akishindwa he always has an excuse.
 
Anyways, katiba imemruhusu kufanya hivyo. Asitegemee kupewa ushindi wa mezani.

Ila baada ya siku 14 hatakuwa na pa kushikilia tena.

Kama anao ushahidi wa kushikika kuhusu kudukuliwa kwa mfumo auweke wazi, na sio kuongea mambo kwa hisia na kuhisi hisi.
 
Sababu inaonyesha Uhuru na Jubilee walikuwa na broad appeal.Wewe jiulize kwani Odinga alishinda vipi urais na kupoteza wabunge na maGavana wengi vile?
Simple logic! Hajawahi kujiuliza hili swali
 
Sababu inaonyesha Uhuru na Jubilee walikuwa na broad appeal.Wewe jiulize kwani Odinga alishinda vipi urais na kupoteza wabunge na maGavana wengi vile?
Bwana wewe, kwani mtu akichagua gavana toka jubilee ni lazima achague Rais toka Jubilee?
 
Back
Top Bottom