Kenya 2022 Raila Odinga asema kupiga marufuku uagizaji mahindi nje ya nchi

Kenya 2022 Raila Odinga asema kupiga marufuku uagizaji mahindi nje ya nchi

Kenya 2022 General Election

LUS0MYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2011
Posts
866
Reaction score
1,109
Mgombea urais na kiongozi maarufu wa muungano wa Azomio Raila odinga amewahaidi wakulima kuwa atazuia uingizaji wa mahindi toka nje ya nchi. Na ikumbukwe kuwa mahindi mengi yanazalishwa na kuuzwa kutoka Tanzania

Kwa akili ya kawaida ina maana hawa wafanyabiashara wa Kenya wanapata mahindi bei chee hivyo wanapopeleka sokoni bidhaa za Kenya zinadoda.
 
UKiwa unatafuta madaraka unaongea kila kitu ilimradi upate kura.
 
Attachments

  • Screenshot_2022-05-13-11-05-04-485_com.twitter.android.png
    Screenshot_2022-05-13-11-05-04-485_com.twitter.android.png
    80 KB · Views: 50
Huyu Riala anataka kuifunga nchi yetu tena wakati mama kahangaika kauifungua?
 
Kwani wakenya wanaagiza mahindi nje kwa utashi wa rais, au uhalisia ndio unawafanya waagize nje? Usishangae ukakuta wananchi walishangalia huo utapeli.
 
Dont mind him. Hii ni politiki tu kuwahadaa wapiga kura. Akishaingia Ikulu atafanya lililo sahihi
Where a politician stands for A and voters stand for B, he will talk B, after getting into power he will turn to B
 
Mgombea urais na kiongozi maarufu wa muungano wa Azomio Raila odinga amewahaidi wakulima kuwa atazuia uingizaji wa mahindi toka nje ya nchi. Na ikumbukwe kuwa mahindi mengi yanazalishwa na kuuzwa kutoka Tanzania

Kwa akili ya kawaida ina maana hawa wafanyabiashara wa Kenya wanapata mahindi bei chee hivyo wanapopeleka sokoni bidhaa za K nienya zinadoda.
Kweli kabisa, hawa millers nchini Kenya wanaipata bidhaa hiyo kwa bei chee nje ya mipaka ya Kenya. Jambo ambalo linachangia sana kwenye masaibu na changamoto, ambazo wakulima wa Kenya wamekuwa wakikumbana nazo. Bei ya juu ya mbolea na bidhaa zingine za aina hiyo, ushuru n.k, n.k, zimechangia pia kwenye kupunguza uzalishaji wa zao la mahindi nchini Kenya.

RAO anazungumza kuhusu kutatua kero zao hizo, ili kuwawezesha wakulima kuzalisha mahindi kwa wingi. Hatua ya mwisho ndio hiyo inayozungumziwa, ya kupiga marufuku uagizaji wa mahindi kutoka nje.
 
Huyu naye ana mawazo ya kizee! Sasa si watakufa njaa! Kila mwaka wanalia ukame!
Jombaa, ukame sio kwamba huwa upo Kenya nzima. Kuna sehemu nyingi ambazo zipo productive sana, 'all year round' na watu wa maeneo hayo, tangia wazaliwe, hawajajua ukame ni nini.
Mahindi yanapandwa kwa wingi sana Tranzoia, Kitale. Ila wakulima walianza kupunguza uzalishaji, kisa bei ya zao ikilinganishwa na gharama ya kupanda. Tena wakulima wengi nchini Kenya wamejikita kwenye ukulima wa kunyunyizia, sio ule wa zamani wa kutegemea mvua.
 
Jombaa, ukame sio kwamba huwa upo Kenya nzima. Kuna sehemu ambazo zipo productive sana, 'all year round' na watu wa huko tangu wazaliwe hawajajua ukame ni nini.
Mahindi yanapandwa kwa wingi sana Tranzoia, Kitale. Ila wakulima walianza kupunguza uzalishaji, kisa bei ya zao ikilinganishwa na gharama ya kupanda. Tena wakulima wengi nchini Kenya wamejikita kwenye ukulima wa kunyunyizia, sio ule wa zamani wa kutegemea mvua.
Mimi kwa mfano sijawahi experience ukame tangu nizaliwe na chakula tunachokula huwa tunatoa shambani wala hatutegemei vyakula vya kutoka nje ya mipaka ya Kenya. Inachekesha sana pale watanzania ufikiria kwamba ukame upo kila mahali Kenya, na kwamba wakenya wote hutegemea chakula cha msaada. Mimi hata sasa hivi kwetu tumeshuhudia mvua tangu mwisho wa mwezi wa tatu and its still raining hadi sasa.
 
Kwenye dunia ya sasa, ambapo kila info inapatikana kwa urahisi, huo mimi huwa nauita upumbavu. Kama sio upumbavu basi ni kimbembele na ujuaji mwingi. Naelewa kwamba hata mtu mwenye PhD zake hawezi akajua kila kitu, kilicho chini ya jua.
Ila mimi huwa nina mazoea ya kufanya karisechi, angalau hata kadogo tu. Kabla nitupie maoni yangu, kwenye mjadala, ambao unazungumzia jambo ambalo sina uhakika kulihusu. Kando na hapo ustaarabu ni kubaki tu kimya, ili ujifunze mapya.
 
Mimi kwa mfano sijawahi experience ukame tangu nizaliwe na chakula tunachokula huwa tunatoa shambani wala hatutegemei vyakula vya kutoka nje ya mipaka ya Kenya. Inachekesha sana pale watanzania ufikiria kwamba ukame upo kila mahali Kenya, na kwamba wakenya wote hutegemea chakula cha msaada. Mimi hata sasa hivi kwetu tumeshuhudia mvua tangu mwisho wa mwezi wa tatu and its still raining hadi sasa.
Ww kwenu ni wapi? Au ni Kisii, coz Najua kule ndio hakuna ukame
 
Hiyo ndio tofauti Kati ya kiongozi na raia, kiongozi anazungumzia wananchi wote, wakati raia anafikiria kuhusu yeye na familia yake. Kama wewe hujawai kukutana na njaa au ukame, Kuna zaidi ya wakenya 3M wapi hatarini kupoteza maisha kwasababu ya ukame, wewe hao hawakuhusu, lakini rais huo ni mzigo wake lazima ashughulike nao.

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Ww kwenu ni wapi? Au ni Kisii, coz Najua kule ndio hakuna ukame
Migori ndio nyumbani. Sio kisii pekee yake ila western Kenya in general inapokea mvua almost all-year round, na huku hakuna siku utasikia kuna uhaba wa chakula ama kwamba wakazi wanategemea misaada kutoka kwa serikali. Hata bonde la ufa sehemu nyingi tu hupokea mvua mwaka mzima. Nakuru county, most parts of Laikipia county, Trans Nzoia County, Usain Gishu county, Bomet County, Kericho County, Nandi County, zote hizo hupokea mvua kwa wingi sana. Ukame upo mostly in lower eastern Kenya, northern Kenya, central and north Rift na baadhi ya maeneo ya pwani na huku ndio hukuanga na tatizo la njaa
 
Back
Top Bottom