Raila Odinga: Tunavyoshambuliwa na polisi sio sawa

Raila Odinga: Tunavyoshambuliwa na polisi sio sawa

Kenyan

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2012
Posts
414
Reaction score
314
Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga kupitia ukurasa wake wa twitter amelalamikia kile alichokitaja kama kushambuliwa na maafisa wa polisi hasa katika eneo la Pipeline, Nairobi ambako msafara wake [kwa mujibu wa picha zilizoko hapo chini] umeshambuliwa kwa nguvu kupita kiasi.

Picha zinaonesha namna msafara wake ulivyoshambuliwa kwa kutumia kanoni za maji huku gari linalombeba Raila likiwa limeharibiwa vibaya kwa kutupiwa mabomu ya machozi.

Raila amemuonya Rais William Ruto na Naibu wake kwa kuandika:

"Siku zenu zinahesabika, na nyie basi muanze kuzihesabu."

Kwa sasa msafara huo upo barabara ya Outering ukijizatiti kuingia kati kati ya Jiji.

20230330_171358.jpg
20230330_171402.jpg
 
Back
Top Bottom