Raila should not be allowed on Live TV

Sisi ndiyo chaguzi zetu zikose hila ?!! Kwa tume hizi za kina Lubuva na huyu jamaa wa Zanzibar nimemsahau jina, mpaka leo anajificha jificha!!! Tz ndiyo hali ni mbaya sema WaTz hawajali sana.

Chaguzi za Africa siyo

Cairo's
TZ ni wajinga wengi
 

Kama unaongelea TZ sisi wananchi hatujasahau yaliyotokea. Haikutokea HATA SIKU moja jamaa wakasema kuwa kuna hata kata moja ambapo kura zilizotangazwa zilitofautiana na kura zilizosainiwa na mawakala. Kama unaamini watu makini wanaweza kudai kuwa wameibiwa bila kudai wameibiwa wapi jifikirie umakini wako pia.
 
Nyie wangapi?Mbona na sisi ni wananchi? Wapi watu waliambia walete ushahidi na lini?Habari za kuambiwa na kujipeleka mbele km vile umeshuhudia ndio maana waafrica kufika mbinguni ni ngumu.Ni waongo hadi kwa nafsi zao, wanaapa kwa niaba za wenzio km vile wenzao ni malaika wa kuminika milele na tk kila kitu.
 
Hii issue ni simple kama Raila amekuwa defeated fairly. Huyo bwana awe heard out then anachodemand kiwekwe mezani. Kama bado ameng'ang'ania 34A forms, shida ipo wapi kuziweka hadharani? Ajibiwe kwa hoja na evidences ili akose hoja. Hao wanaolianzisha ni kwa sababu hawaoni majibu sahihi yakitolewa.
 

Usijitoe ufahamu ndugu yangu. Mtu akilalamoka kuibiwa haulizwi umeibiwa shilingi ngapi. Sema kura zangu kata hii zilikuwa kadhaa halafu tume ikatangaza kiasi hiki ambacho ni pungufu. Sasa kusema nimeibiwa bila ufafanuzi ni watu wa ajabu tu watakaokutilia maanani. Suala la kuambiwa ulete ushahidi ni baadaye. Baada ya kusema kura zilikuwa 27 lakini zikatangazwa 23 hapo ndio ushahidi utatakiwa sio kabla ya kutoa hoja. Hoja ni kuwa kura zangu jimbo fulani zimepunguzwa kiasi cah kura 10. Hapo waweza kuambiwa ulete ushahidi. Kusema tu nimeibiwa kura bila kutaja ngapi na wapi ni ngonjera ambazo zitatiliwa maanani na waliojivua ufahamu tu.
 
Unajifanya kichaa ili usamehewe. Nini hujaelewa?Wapi Loawasa aliambiwa alete ushahidi akakataa? Na hata angeleta ushahidi unafahamu sheria ya bongo baada ya tume kutangaza kwa matokeo ya uraisi? Sasa habari za wanasesere unamletea nani hapa.Kushindwa kwako kutafsiri hoja kusiwe sababu ya kulazimisha ujinga kuwa sahihi.
 

Jitahidi kujitoa ufahamu. Na dalili ya mtu kujitioa ufahamu ni kutukana kama unavyofanya. Habari ni kuwa Lowassa hakuwahi kulalamika bali alisema ngonjera zake na kadhalika. Kulalamika ni kusema sehemu fulani kura zangu zilikuwa 10 lakini zikatangazwa 7. hayo ndio malalamishi. Kusema kuwa nimeibiwa bila kutaja nini ni kutoa ngonjera. Na angelalamika kihivyo kuwa kura zimepunguzwa jimbo au kata fulani NI LAZIMA angeambiwa atoe ushahidi. KWA TAARIFA yako wasingeweza kutoa data za uongo kwa sababu sheria inakataza na wangekuwa wamefanya jinai kama wangetoa data. Badala yake wanadhani WaTZ wote ni manyumbu kuwa wakisema tumeibiwa na wote watawasikiliza.Wamelalamika bila data kwa kuogopa sheria. Kama bado hujaelewa nakuruhusu uendelee kutoa matusi na kutukana na kutukana kwa sababu ndicho unachoelewa na labda umeajiriwa kufanya hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…