Jay456watt
JF-Expert Member
- Aug 23, 2016
- 10,356
- 7,992
Kwa mtazamo wangu, kuondoka kwa Raila kutazuia ghasia na vita ambavyo vingeibuka baada ya uchaguzi wa Oct 26. Tayari IEBC wameshasema kuwa hawatofanya mabadiliko ambayo NASA ilikuwa ikiamrisha na kwa hiyo kama Odinga angeshindwa tena katika uchaguzi wa pili, bila shaka wafuasi wake wangezua rabsha haswa katika maeneo ya Kisumu, Mathare na Kibera. Kwa sasa Odinga hawezi akathubutu kulaumu yeyote sababu amejitoa mwenyewe toka kinyang'anyironi bila ya kuambiwa na mtu yeyote. Kwa mtazamo wangu, uamuzi huo ndio ulikuwa mwisho wa uwepo wake katika siasa za Kenya. Uchaguzi unaweza ukaandaliwa hata ikiwa Kenyatta hana mpinzani. Kujitoa kwake kunaleta taharuki ya kikatiba ila kwangu mimi naona it is the best thing for Kenya. Itazuia vita na kuathirika kwa uchumi. Hakuna chochote kile ambacho kingezuia vita baada ya uchaguzi wa Oct 26. wafuasi wa Odinga huwa very violent and to some extent, unreasonable. bila shaka wangezua rabsha tu hata KDF, SWAT na FBI wakipelekwa kule. Damu lazima ingemwagika.
Forgive my Swahili. I gave it my best shot.
Forgive my Swahili. I gave it my best shot.