Raimu Ya Katiba,SURA YA SITA MUUNDO WA JAMHURI YA MUUNGANO,ongelea kidogo kwa kutoa maoni

Raimu Ya Katiba,SURA YA SITA MUUNDO WA JAMHURI YA MUUNGANO,ongelea kidogo kwa kutoa maoni

Kimetah

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
1,049
Reaction score
189
Muundo wa Muungano
57.-(1) Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye
serikali tatu ambazo ni:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na
(c) Serikali ya Tanzania Bara.
(2) Shughuli za Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kusimamiwa
na:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(b) Bunge la Jamhuri ya Muungano; na
(c) Mahakama ya Jamhuri ya Muungano.
(3) Muundo, madaraka na mambo mengine ya kiutendaji yahusuyo
Serikali yaTanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yataainishwa
katika Katiba za Washirika wa Muungano

Vyombo vya utendaji vya Jamhuri ya Muungano

58.- (1) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa ndiyo chombo
chenye mamlaka ya utendaji, Bunge litakuwa na mamlaka ya kutunga sheria
kwa mambo ya Muungano na kusimamia utekelezaji wa shughuli za Serikali
ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama itakuwa ni chombo cha utoaji haki.


(2) Kila chombo kilichotajwa katika ibara hii kitaundwa na kutekeleza
majukumu yake kwa kufuata masharti ya Katiba hii.
 
Back
Top Bottom