mwananthropolojia
JF-Expert Member
- Oct 6, 2012
- 956
- 657
tumekuwa tukiona jinsi ,wabunge wetu wanavyojaribu kuwawajibisha mawaziri wetu wanaosema uongo katika bunge,na hii imesaidia sana kuleta uwajibikaji kwa kiasi fulani ingawa tumekuwa tukiona wakikingiwa vifua na maspika wetu wababe,ila sijawahi kusikia raisi akidanganya kama naye bunge letu linaweza kumwajibisha, kwani katika katika mfumo wetu wa check and balance ,bunge linakua linaitazama serikali isfanye uozo na kuwajibika kweli kwa wananchi waliowachagua kuwatawala.
swali nililonalo ni je raisi ambaye ndiye mkuu wa serikali akidanganya umma anaweza kuwajibishwa?ingawa mkuu wa shughuli za serikali bungeni ni waziri mkuu, raisi anawajibika kwa nani? na kama hawajibiki kokote napendekeza kwenye katiba ijayo naye ajumuishwe akisema uongo kwa wananchi hata kama ni majukwaani ili mradi alikuwa kwenye shughuli za uraisi basi kupitia kwa wawakilishi waliochaguliwa na wananchi ambalo ni bunge nao wamwajibishe.
na maspika kazi zao ziwe kusimamia bunge na sio nao kushiriki katika majadiliano na ubishani ndani ya bunge