Rais akiliweka suala la wawekezaji kama 'fungulia mbwa', sijui nini kitatokea

Bora irudi kwa JK kuliko enzi za jiwe
Yaani Mpango inabidi afanye kazi yaziada kuzuia haya mawekezaji majizi, akiamua kumfuata mama asilimia 100% tunarudi kule kwa JK nanchi itabakia mashimo.
 
Baada ya kampuni ya Airtel kuwarudishia hisa zenu bei ya bando imeshuka??
 
Baada ya kampuni ya Airtel kuwarudishia hisa zenu bei ya bando imeshuka??
Gharama za uendeshaji kampuni ya mawasiliano sio mdogo. Kila baada ya miezi 18 teknolojia ya mawasiliano inabadilika, na wao inabidi wajipange kwenda na wakati. Lasivyo usingepata fursa ya kujibu nilichoandika hapa kwa kukosa mtandao wenye uhakika.
 
Tangu lini Chadema wakaitakia mema ccm hadi wajipe kazi ya kumsifia rais Samia?.

Kazi ya kumsifia rais Samia ni ya MATAGA siyo ya chadema
 
Hao wawekezaji mnaombiwa Walikimbia nchi Walikimbilia Mozambique,zambia or Uganda , all corrupted countries, waambieni wakimbilie Kenya kama hawaja nyooshwa na kodi, mwekezaji aje lakini ambae analipa kodi ili nchi iweze kujiendesha, hivi jamani mwekezaji au mfanya biashara hataki EFD huyu ni mfanya biashara kweli? tusijidanganye kurudi kule tulikotoka ni kubaya, TRA watoe tu elimu ya kutosha kwa wafanya biashara tuendelee kulipa kodi.
 
Huu muda uliopoteza kuandika ngonjera ungekunywa hata mbege. Uko nyuma sana ya muda, Amka.
Inasikitisha sana.Mbaya zaidi hayo mambo si muhimu kuyaweka hadharani kuna mambo mengine yalipaswa kuzungumzwa ofisini maana ukiweka hadharani yanabomoa zaidi kuliko kujenga na ndiyo maana JPM siyo kwamba hakutambua bali alitambua kuwa kuweka kila kitu hadharani itampotezea focus yeye pamoja na serikali yake.Lakini huyu mama hajatambua hilo bado.

Pumzika kwa amani JPM
 
Unapozungumzia hizo awamu ukumbuke kwamba awamu ya Nne ilikuwa na miaka Kumi na awamu ya Tano ilikuwa na miaka Sita tu!
 
Eeh Mungu Mwenyezi, tunaomba utuhurumie tena Tanzania😭😭😭! Lisiwe tena pango la wanyamg'anyi🙏🙏🙏! Tunaomba eeh Mwenyezi Mungu!
Wanyang’anyi walikuwa Magufuli na vijana wake kina Sabaya. Na Mungu ameshstusaidia kwa kumfutilia mbali huyo Magufuli kwenye uso wa dunia
 
Kama alikuta nchi imeoza yeye amefanya nini??? Mbona uwekezaji ndo umekufa??? Watu hawana ajira kwa sera zake mbovu??? Makampuni yamefunga biashara na kuondoka??? Mbaya zaidi kwa miaka 5 tu aliyokaa madarakani akakopa kuliko miaka 10 yote ya mtangulizi wake??? Alifanya lipi la maana????
 
Kwendeni zenu ilani ya chama ni ile ile Mama anatembea nayo, hata wakati anaondoka JK mabadiliko ya hapa na pale yalikuwepo tuvumiliane kaeni SUB hapo benchi kwanza ili mambo mengine yaendelee.
 
Unapozungumzia hizo awamu ukumbuke kwamba awamu ya Nne ilikuwa na miaka Kumi na awamu ya Tano ilikuwa na miaka Sita tu!
halafu leo mtu anakwambia eti jpm amefanya nini?!!...tofauti ni kubwa sana kati jpm na jk ...jpm vitu vingi vya maendeleo vinaonekana kwa macho bila hata kuuliza ndani ya miaka 5 tu .jk miaka 10 tunaambiwa nchi haina uwezo,umeme hkn,watu wanagawana pesa kwenye masandarusi,rais full kutembea ulaya leo yupo america anapiga picha na boyz to men kesho yupo sijui wapi,ujambazi ukashamiri,madawa ya kulevya eti leo turudi huko thubutu !!! ...wauza ngada na watu wenye maslahi yao ya kuliangamiza taifa kwa manufaa yao binafsi kamwe hawataweza na hata huyo mama akielekea huko atakumbana na nguvu ya umma tu
 
Tanzania haijawahi kuacha kuwa pango la wanyang'anyi. Sarakasi zote za jiwe kwa Barick ziliishia kupata kishika uchumba tu.
Lakini alizuia Makinikia kwenda nje, hapo vipi?
 
Umakini unahitajika sana katika maamuzi ya mambo makubwa na yenye maslahi kwa Taifa kama ulipaji kodi na Issue ya wawekezaji, vinginevyo tutarudi kule kule kwenye SHAMBA LA BIBI aka BUSINESS AS USUAL.
Tukumbuke, JPM amejitahidi sana kulinda, kutetea na kuendeleza rasilimali za Taifa hili. Amejitahidi sana tena sana.
 
Unataka kutuambia unajua mengi mno kupita Rais Mama Samia?[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848] basi ni Maajabu na dunia inaelekea mwisho yaani fukara wa mtaani kama wewe ni zaidi ya Rais?
Mwehu huyo, walitaka kupiga wao kwa kisingizio cha mwekezaji wa ndani. Majangili wakubwa hao. Shubaaamit
 

Ukiunda biashara ambayo iko kwenye misingi ya kukwepa kodi na kilaghai mapato yake unategema hiyo biashara itadumu ndani ya mfumo wa kulipa kodi halali na kupata leseni kihalali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…