Rais alipaswa kujiuzulu baada ya report ya CAG

Rais alipaswa kujiuzulu baada ya report ya CAG

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2018
Posts
2,754
Reaction score
4,975
Baada ya report ya CAG kuweka wazi wizi na madudu yanayoendelea huko serikalini, Kiongozi makini na mzalendo alipaswa kukaa pembeni kupisha uchunguzi.
Lakini tujiulize, Kiongozi aliyeteleza kwa kuzungumza hadharani, iwe kwa ukweli au kwa uongo kwamba "kuna siku nchi itapigwa mnada kwa madeni" Lakini akalazimishwa kujiuzulu, Je, Vipi kuhusu yule anayeruhusu na kuidhinisha mabilioni ya watanzania wanaoteseka na umasikini maradhi na ujinga yaibiwe? Yupi haswa aliyepaswa kujiuzulu?
 
Rais ameshaagiza Wezi wote washughulikiwe

Ni jukumu la Bunge kutuambia nani na nani wanafikishwa kwa DPP
Kwa hiyo ni "jambo kubwa", au siyo; hadi Rais kaamua kufanya hivyo!

Sasa hilo la "Rais kuagiza wezi wote washughulikiwe", ni jambo tofauti tunaloweza kulijadili kama liko sawa au haliko sawa, baada ya kukubaliana kwamba "Mnakuza sana mambo" kama ulivyosema mwanzo haikuwa sahihi.

Hili la "...Bunge kutuambia..." sijui kama ndio utaratibu mahsusi wa kushughulikia wezi, lakini ngoja tusubiri, hakuna haraka, tuone watakavyoshughulikiwa.
 
Kumtaka Rais ajiuzulu ndio kukuza jambo huko

Spika Tulia: CAG ni jicho tu la Bunge lakini hana mamlaka ya kuifanya maamuzi yoyote
 
Kumtaka Rais ajiuzulu ndio kukuza jambo huko

Spika Tulia: CAG ni jicho tu la Bunge lakini hana mamlaka ya kuifanya maamuzi yoyote
Hapana.

Wizi wa mali ya wananchi ni jambo kubwa sana ambalo hata Rais anapaswa kuwajibishwa kama siyo kuachia ngazi mwenyewe ikibainika kwamba kafanya udhaifu kwenye eneo hilo. Ni jukumu lake kuhakikisha kwamba mali za wananchi hazichezewi. Ndiyo maana anapewa vifaa vyote hivyo vya kutendea kazi. Ni jukumu lake kuvisimamia vyema na kuhakikisha vinafanya kazi ipasavyo.

Kwa hiyo ni jambo kubwa linaloweza kusababisha yeye mwenyewe ajiuzuru au hata kufikishwa mahakamani kama kahusika na wizi (usiniambie habari za Katiba mbovu).

Tunachoweza kukubaliana hapa ni kuwa acha Bunge litafute ukweli ulivyo.

Habari ya jambo kuwa kubwa hilo tumekwisha limaliza.
 
Marais na viongozi wanaojiuzulu mostly ni wale ambao wananchi husika ni wazalendo na makini, wasiotayari kuvumilia madudu yakitendwa juu ya fedha na mali za nchi yao.

Tanzania mbona ni shamba la...!!!
 
Marais na viongozi wanaojiuzulu mostly ni wale ambao wananchi husika ni wazalendo na makini, wasiotayari kuvumilia madudu yakitendwa juu ya fedha na mali za nchi yao.

Tanzania mbona ni shamba la...!!!
Nasi siku moja tutafika huko tukishachoshwa na upuuzi huu uliopo sasa.
 
Nasi siku moja tutafika huko tukishachoshwa na upuuzi huu uliopo sasa.
Hata kile kizazi cha ^Juliasi^ kilisemaga hiko kitu kama wewe tu hapo. Let the change begin with you! It can be done, play your part! Au unaogopa?
 
Hata kile kizazi cha ^Juliasi^ kilisemaga hiko kitu kama wewe tu hapo. Let the change begin with you! It can be done, play your part! Au unaogopa?
Hicho kizazi huwezi kukilinganisha na hiki kilichopo leo; pamoja na kwamba hakikuwa na wasomi wengi, lakini watu walijitambua vizuri sana, siyo kama leo hii.
 
Back
Top Bottom