Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Hapa juzi nimeona taarifa Rais Samia akiwaambia wananchi wa Kilosa wamrudishie Prof. Kabudi katika uchaguzi wa 2025. Nimejiuliza sana bila kupata jibu, kama Rais Samia haoni ni kosa kubwa sana kwake, kuwaambia wananchi nirudishieni Prof Kabudi, au kiongozi yeyote wa CCM, mwaka 2025?
Rais Samia anaposema nirudishieni kiongozi fulani aliyepo madarakani mwaka 2025, haya yanajitokeza;
Reherence: Samia ampigia chapuo Profesa Kabudi kiaina
Rais Samia anaposema nirudishieni kiongozi fulani aliyepo madarakani mwaka 2025, haya yanajitokeza;
- Haheshimu utashi wa wananchi kwamba wanaweza wakawa hawamtaki kiongozi aliyepo, hata kama ni waziri
- Anawaambia watu wengine watakaotaka kutia nia kuwania nafasi hizo za CCM kwamba nafasi hizo tayari zina wenyewe
- Haheshimu utaratibu CCM iliyojiwekea wa kuwapata viongozi kwa kuanza na kura za maoni na anaona yeye ndie anaepaswa kuwaambia nani anataka awe kiongozi au wamrudishe
- Tayari amejihakikishia kwamba yeye ndio Rais ajae 2025 japo uchaguzi bado
Reherence: Samia ampigia chapuo Profesa Kabudi kiaina