Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Ukisikia dharau, hii imepita kiwango cha kawaida cha dharau.
Rais Samia na 4R zake Kila anakopita anahimiza Wananchi kujitokeza kuboresha Taarifa zao kwenye daftari la Wapiga Kura na àmbao hawana vitambulisha kutokana na umri au vimepotea wachukue vipya. Kisha anamalizia Kwa kuwataka wajitokeze Kwa wingi October 2024 na 2025.
Moja Kati ya aibu kubwa na jinsi jinsi uongozi unavyokosa kuheshimika ni pale unapochaguliwa na wapiga Kura wachache huku wengi wakikataa kwenda kupiga Kura wakati Wana sifa zote. Tuchukulie nchi ina wapiga Kura milioni 32, lakini waliojitokeza kupiga Kura ni milioni 7. Rais anasinda na mil.5 ambayo ni 71.4% ya waliojitokeza kupiga Kura. Kwa macho ni ushindi mkubwa, lakini kumbuka watu mil.5 ni asilimia 15.6 tu ya wapiga Kura Mil.32. Uwiano huu kisiasa utampa mtikisiko mshindi hata kama atajikaza na kusema nimeshinda kihalali.
Wakati Rais akihimiza watu kupenda kushiriki uchaguzi ghafla anajitokeza Mteule wake na kauli za "kipuuzi" alizozoea na kuwaambia wapiga Kura kwamba hata wajitokeze kupiga Kura, wao si muhimu kuliko Wasimamizi wa uchaguzi wanaohesabu na kutangaza matokeo. Kiufupi ni dharau Kwa wapiga Kura kwamba si lazima mliyemchagua atangazwe kuwa mshindi Bali ushindi unategemea matakwa ya msimamizi wa uchaguzi na aliyemteua.
Kama Mh Rais atanyamazia hili bila kuchukua hatua ya kumwajibisha Msemaji basi Wananchi wajue kauli ya Nape ina baraka za Mteuzi wake japokuwa sitaki kuamini hilo.
Mara nyingi nimekuwa nikisema yawezekana Samia alikuwa na nia njema Sana na demokrasia ya Nchi hii mara alipochukua Urais. Lakini ghafla Kwa Udhaifu WA kibinadamu akapelekewa lundo la ushawishi wa ovyo toka Kwa watu kama Nape na ghafla akaanza kukamata Wapinzani, kupuuza madai ya katiba mpya nk.
Mimi ni Tomaso, nasubiri kuona.
Soma=> Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Kauli ya "Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza" ilikuwa ni ya utani