Rais anapata wapi mamlaka ya kuagiza Spika asilipe posho za Wabunge?

Jielekeze kwenye hoja, suala siyo posho. Tunajadili mamlaka ya Rais dhidi ya Bunge na Mahakama, ni sahihi kwa muhimili mmoja kutoa MAAGIZO kwa mihimili mingine?
Mwisho wa maelezo yangu nimekuandikia kwamba rais ni mkuu wa nchi na mkuu wa serikali. Tatizo ni kugundua ni wakati gani anazungumza kama mkuu wa nchi na wakati gani ni mkuu wa serikali.
Siku akisema tujifungie ndani kwa sababu ya Coronavirus, hata Bunge halitakaa. Sasa usiulize kwa nini Bunge halikukaa wakati Spika hajasema.
 
Hapo ndipo inapojidhihirisha nadharia ya UTAWALA WA MKONO WA CHUMA, na DANGANYA TOTO YA mihimili mitatu inayojitegemea kimaamuzi. Umeelewa sasa?
 
Hapo ndipo inapojidhihirisha nadharia ya UTAWALA WA MKONO WA CHUMA, na DANGANYA TOTO YA mihimili mitatu inayojitegemea kimaamuzi. Umeelewa sasa?
Kwani shida nini? Wewe ni Mbunge uliyetaka kuendelea kupata posho pamoja na kwamba huingii Bungeni? Mawasiliano ya Mihimili mitatu unayoitaja ktk nchi kila wakati yapo na makubaliano yapo. Kama hiyo mihimili haiwasiliani basi, hiyo siyo nchi. Tatizo ni kwamba ulisikia jinsi rais alivyozungumza lakini kama angekaa kimya usingeelewa.

Huo uhuru hutaupata boss! Hata iwe US! Si unasikia DP anavyopapulana na spika Nancy? Hiyo mihimili iko wapi na uhuru uko wapi?
 
Inaonekana unatetea bila kujua kinachojadiliwa hapa. Hizo SMARTPHONE mlizogawiwa ili kutetea jiwe zimewafanya mmekuwa na akili za hovyo namna hii?
 
Mimi mbona nilishaamka usingizini kwamba ikulu ndo kila kitu
 
Mtoa hoja hajahalalisha wana-CDM KUJICARANTINI, wala hajawatetea kwamba walipwe posho bila kuhudhuria vikao! Hoja yake ni; je muhimili unaweza KUAGIZWA na muhimili mwingine kulipa au kutolipa posho?
La pili nnalo liona niiii, linatakiwa AGIZO, au kuna kanuni elekezi kwamba ukijikarantini itakuaje? Kama hujashiriki vikao vya bunge, sheria na kanuni zinasemaje?
 
Inaonekana unatetea bila kujua kinachojadiliwa hapa. Hizo SMARTPHONE mlizogawiwa ili kutetea jiwe zimewafanya mmekuwa na akili za hovyo namna hii?
Elimu duni boss! Mtu akikutoa nje kidogo tu unapotea. Kwa hiyo nijadili posho za wabunge na nani atoe amri? Is such a discussion productive in anyway to guarantee wastage of my time? Jitahidi uijue dunia badala ya kuhangaika na CHADEMA-CCM-CUF-TLP, and other sorts of rubbish! That is what we call poor education that has failed to replace an empty mind.
 
Inasikitisha sana, Tume ya uchaguzi kuwekwa MFUKONI NA RAIS kutoka chama cha CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…