Rais anaposema "Ngwini" ana maana gani?

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,409
Reaction score
13,262
Katika onyo lake kuhusu watu wanaotoa takwimu zinazotofautiana na zile za idara ya takwimu ya taifa, rais amesema "... unakuta ngwini mmoja amebobea huko anatoa takwimu kwamba anajua kutengeneza takwimu .... Alikuwa ana maanisha nini?
 
Hahahahahah
 
Kuna ngwini mwingine Ikulu inadaiwa ana Phd ya kuchoma korosho ila watu walioutafuta ushahidi wanadai hakuna uthibitisho wa hilo.

Ha haa! Nimechekajee?
Ngwini ni lugha ya chuoni (hasa UDSM).
Ngwini ni mtu anayesomea masomo ya arts yale ya kukariri yasiyo na michoro wala hesabu!
 
Nyambari Nyangwine,,,watu wablabla tuu wasio tumia nguvu sana kutafakari kila kitu wameshatafuniwa
 
Katika onyo lake kuhusu watu wanaotoa takwimu zinazotofautiana na zile za idara ya takwimu ya taifa, rais amesema "... unakuta ngwini mmoja amebobea huko anatoa takwimu kwamba anajua kutengeneza takwimu .... Alikuwa ana maanisha nini?

Katika onyo lake kuhusu watu wanaotoa takwimu zinazotofautiana na zile za idara ya takwimu ya taifa, rais amesema "... unakuta ngwini mmoja amebobea huko anatoa takwimu kwamba anajua kutengeneza takwimu .... Alikuwa ana maanisha nini?
....

Acha UNGWINI mkuu
 
.
Anamaanisha wale waliosomea masomo ya arts. Zamani walitumia vitabu vilivyochapishwa na penguin house (Ngwini) vya Uingereza.

Katika masomo ya sayansi tokea mwanzoni kabisa mtu anafundishwa jinsi ya kutumia vipimo au data kufafanua na kuonesha njia ya kupata jibu pamoja na kujua limits.

Utakuta mtu akifikia elimu ya chuo kikuu teyari utaratibu huo kwake ni wa kawaida na hawezi kukosea. Sasa Mh. Rais alikuwa anampiga mtu dongo ambaye ni 'NGWINI' kwa kufanya makosa ya kutumia data bila kujua msingi wake na kuziwasilisha jumla jumla.
 
Katika onyo lake kuhusu watu wanaotoa takwimu zinazotofautiana na zile za idara ya takwimu ya taifa, rais amesema "... unakuta ngwini mmoja amebobea huko anatoa takwimu kwamba anajua kutengeneza takwimu .... Alikuwa ana maanisha nini?
Neno ngwini ni terminology ya zamani UDSM ikimaanisha "Penguin" na hao ni watu waliosomea masomo ya arts. Penguin ni kampuni ya uchapishaji vitabu.
 
Hahahaaaa...ngwini hajui hesabu sasa ataweza vipi kuchanganua takwimu ambapo ndani yake kuna hesabu?
Ole wake ngwini atakayejifanya kuchambua takwimu za BOT, NBS.... onyo ndo limetolewa hivyo.
 
Nikajua kachapia kwamba alimaanisha ngwiji
 
Ha haa! Nimechekajee?
Ngwini ni lugha ya chuoni (hasa UDSM).
Ngwini ni mtu anayesomea masomo ya arts yale ya kukariri yasiyo na michoro wala hesabu!
From the world Penguin --- wale publishers maarufu wa vitabu duniani. Mara nyingi wao wakipublish manovo vovo meengi.
 
Mtu aliebobea kwenye Gwini ni Mbobezi wa Masomo yasiyo na hesabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…