Rais Assad aripotiwa kuikimbia Syria, Majeshi ya Waasi yatangaza kuuchukua mji mkuu wa Damascus

Hili lijamaa lililoongoza haya mapinduzi linaonekana lina akili labda libadilike huko mbeleni. Linasisitiza wapiganaji wasilete fujo kwa raia na limewapiga marufuku kusheherekea kwa kwa kupiga risasi hewani. Ngoja tuone kimbembe kipo kwenye kuunganisha makundi mengine ya wapiganaji
 
Kiuhalisia hili la waasi kufanikiwa kwa haraka haraka hapo Syria hata mimi limenishangaza sana, inaonekana dunia inakwenda kasi sana kwenye mambo mengi na kuna vitu vingi mnoo vinaendelea chini kwa chini hapa duniani na hatuvijui.

Waliomsaidia miaka 10 iliyopita yaani Urusi, Iran na Hizbollah wako busy na mambo yao yanayowahusu.
 
Hakuna Cha maana inakwenda kuwa kama Libya tu.kila mtu atataka kuongoza
Libyia ilikuwa na mgawanyiko sabab waas walianza muua Ghadaf ikiwa bado jeshi la serikali lina nguv na target ya West ilikuwa kumuondoa Ghadaf tu hawakuwa na malengo zaid , ila Syria kila mtu anahitaj kupatawala so lzm hao waasi watabakia kupatawala nankusetle amani ili watu msianze kumkumbuka Assad
 
Syria huenda ikawa kama Sudan, baada ya Omar Al Bashir kuondolewa madarakani, hadi leo ni mapigano, pia Libya au Iraq na mashaka sana huenda Syria itaelekea mkondo huo..!!

Mimi naona bora amepinduliwa sbb inakumbusha watawala wengi wa sasa duniani kuwa Uongozi bora ni kuwatumikia watu kwa kuwa tendea mema na kuwajali na sio kuwatumikisha watu kama watumwa..!! Kuna mstari mwembamba sana unaotofautisha viongozi wanao watumikia watu na kuwajali watu wanao waongoza na viongozi wanao watumikisha watu kama watumwa.
 
Mrusi anawekwa busy makusudi, yuko too expanded kwa sasa hawez saidia washirika wake kimamilifu
Mrusi aliustukia mchezo kitambo akamuonya Assad juu ya Erdogan na mpango mzima wa NATO.

Kinomuondoa Assad Syria ni msimamo wake wa kuendelea kuwasaida Iran na Hezbollah kupitisha silaha kwenye ule mji wa Qusayir.

Sasa hizi Hezbollah wameondoka hapo Qusayir na HTS wameingia hapo hilo ndo lengo la Israeli.

Lakini bado vita kali itapigwa kati ya magaidi na Israeli pamoja na Uturuki kugombea Damascus.
 
Lakini cha ajabu ambacho wengi twashangaa ni kwamba HTS ni magaidi kwamba ni generation ya ISIS.

Sasa iweje leo waaminike kufanya kazi waloifanya na je watakubali kuachia uongozi wa kiraia Syria?
Ugaidi ni suala la mtazamo tu.

Kuna kipindi hata Al Qaeda walikuwa ni washirika wa Marekani, enzi za uvamizi wa USSR huko Afghanistan.

Hata ANC kuna kipindi ilikuwa designated kama kundi la kigaidi.

Leo hii ANC ni chama tawala AK.
 
Syria huenda ikawa kama Sudan, baada ya Omar Al Bashir kuondolewa madarakani, hadi leo ni mapigano, pia Libya au Iraq na mashaka sana huenda Syria itaelekea mkondo huo..!!

Inaelekea huko. Sema Hawa majamaa inaonekana kuna kitu wanacho. Wanaweza kuongoza kwa muda mrefu.
 

Uturuki itapiganaje na waasi?. Wao ndio wanawasapoti
 
Mwisho wake umefika, hana jinsi yoyote ya kumbakisha madarakani.

Ila hii oparesheni ya waasi imenishangaza sana, ndani ya muda mfupi wamechukua nchi!
Yalishapangwa hayo tuko nyakati za mwisho kuelekea NWO, ila Wakristo wa Syria watamkumbuka sana Assad, leo hi I unamtoa Assad mnawaweka ISIS, il Israel iweze kuongeza Ardhi kusini mwa Syria😀
 
Hapawezi kutulia
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…