Rais ataendelea kufumua baraza la mawaziri mpaka lini?

JATELO1

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2011
Posts
1,230
Reaction score
301
WANAJF;
Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana kuhusu hili suala la Mh. Rais Kikwete kufumua Baraza la Mawaziri mara kwa mara, hivi tatizo ni nini? Je, ni kweli kwamba Mh. Rais huwa anakosea ktk teuzi zake? Mimi napata shida sana kuamini hilo na badala yake naamini kwamba ndani ya CCM hakuna mwenye ubora wa kusimamia ofisi za Umma. Na kama wapo, basi ni wachache sana na hivyo inakuwa vigumu sana kwa Mh. Rais kuweza kuwabaini hao wachache ndani ya wengi ambao hakika wana malengo mabaya na utendaji wao una walakini.


Pia naamini kwamba watu wengi sana wenye uwezo na makini hawako ndani ya CCM kwa sasa.

Nawasilisha.

TELO.
 
Inatia hasira na huzuni kwakweli. Labda anakamilisha usemi wake 'maisha bora kwa kila mshkaji wake'. Kwani ni nafasi nyingine kwa sura mpya 'kupiga' hela za nchi yao.
 
Ndugu hapa ni Jukwaa la sheria. Hiyo thread peleka Jukwaa la Siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…