Rais atoe amnesty mafao waliodaiwa kufoji vyeti

Rais atoe amnesty mafao waliodaiwa kufoji vyeti

Nsimbi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
1,091
Reaction score
1,203
Huruma ya Mkuu wa nchi inahitajika mahala pengi hasa ukizingatia mazingira ya mkosaji.
Familia zinapata shida wazazi wanapoachishwa kazi.
Ni kweli Wafanyakazi waliokuwa wamefoji vyeti vya shule walifanya kosa lakini mfumo wa hovyo uliotawaliwa na rushwa ndio wa kulaumiwa zaidi.
Kujuana na upendeleo ndivyo vilivyowapa mwanya wafanyazi hao kughushi hati hizo hasa baada ya kuona hata mabosi wao wanatumia vyeti vya form iv vya marehemu ndugu zao nk.
Uozo ndani ya mfumo wa Serikali umewafanya watu kuchukulia mambo kirahisi mno.
Bado kuna wafanyazi wasio na vyeti halali vya form four katika mfumo wa ajira za umma na hao waliobainika wamefanywa kama scapegoats tu.
Kuna baadhi ya hao waliobambwa kwa kufoji vyeti walikuwa na wachapa kazi wazuri na wamelitumikia taifa kwa muda mrefu. Sawa walikosea kufoji lakini kuna watumishi waliwahi kufanya makosa makubwa zaidi na bado wanadunda.
Kati ya hao wanaodaiwa kufanya kazi kwa kuajiwa kwa vyeti bandia wapo waliokaribia kustaafu na walikuwa wakikatwa kodi ambayo Serikali iliitumia kujenga nchi.
Isitoshe walikuwa wakikatwa michango ya mashirika ya hifadhi ya jamii. Kuwaondoa bila kuwalipa mafao yao ni ukatili mkubwa.
Tayari wamekwisha tumikia adhabu ya kuondolewa kazini. Inatosha. Nawaonea huruma wale waliobakiza miezi michache kustaafu. Jambo hilo limeleta kilio kwa kaya nyingi. Unamnyimaje mafao mtu aliyelitumikia taifa kwa miaka 30?! Rais ashauriwe tena kutoa msamaha kwa hawa jamaa. Mkuchika walipeni bwana na baada ya hapo state izibe mianya yote ya kughushi vyeti ndani ya mfumo wa Serikali.
Tatizo limetengenezwa na jamii yenyewe kutokana na utepetevu wa Serikali katika kupambana na rushwa. Pambaneni na misangara ya ufisadi kwanza ndipo mtakuwa na moral authority ya kuwatunishia misuli wafanyazi wanyonge.
Nanyi Watanzania acheni kushabikia kughushi vyeti. Wazazi wahimizeni watoto kusoma kwa bidii ili wapate maarifa na vyeti halali. Hakuna njia ya mkato.
 
Back
Top Bottom