Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
Ningefikiria zaidi juu ya kazi ya Urais kuwa na muda wa kutulia zaidi ofisini licha ya shughuli za kila siku za Rais ofisini, hii itampa muda zaidi wa kuyapitia mambo mbalimbali yahusuyo uamuzi wa rais na mambo mbalimbali ya serikali kabla ya kutoa uamuzi.
Mambo mbalimbali ya mikataba na mengineyo kwa nchi yetu ni mengi sana, kabla ya kupelekwa bungeni na draft za mikataba rais awe ameyapitia na kujiridhisha pamoja na kuwa na washauri wenye upeo kwa nafasi ya yanayohusiana nayo.
Maamuzi na utekelezaji mbalimbali wa shughuli za serikali katika uongozi yahitaji sana muda wa kutulia, kusoma, kuchambua na kupata ushauri wa washauri waliobobea kabla ya utekelezaji.
Mambo yenye kugusa wananchi moja kwa moja ingefaa yapitie kwa wananchi ili kupata maoni yao.
Naona mara nyingi kiongozi wa nchi yupo katika safari za ndani ya nchi na ziara za nje ya nchi na hivyo muda mwingi kuwa safarini badala ya kukaa ofisini, baadhi ya safari ingefaa zifanywe au kukaimishwa kwa walio chini yake ambao humsaidia kazi ya utumishi na uongozi, lasivyo anakuwa na majukumu mengi ambayo huenda yanamchukulia muda mwingi kuwa nje ya mazingira ya kiofisi, hayo yangekaimishwa kwa wasaidizi wake angeweza kuwa na muda wa kutulia zaidi ofisini kwake.
Kwa maamuzi na utekelezaji wa mambo mbalimbali yahitaji sana kufanya tafakari ya kutosha wakati ametulia ofisini ili kujiridhisha baada ya tafakari na tathmini zaidi ili kusaidia kupunguza kasoro ziwezazo kujitokeza kama za teua tengua, kuteua waliokufa na uhakiki wa drafti za mikataba, etc
Huenda Raia anayashtukia yameshapitishwa bungeni au idara ya serikali. Kwa hitajika usimamizi mathubuti kwa mazingira ya sasa.
Sina hakika kabla ya kutia sahihi kama huwa anapitia kuyasoma yote kabla hajadoshoshea wino.
Kwa kipindi cha mpango wa maendeleo kwa miaka 25 ijayo, Tanzania tuitakayo twahitaji kufanya maamuzi sahihi ya uendeshaji nchi kisheria na kuondoa kasoro zinazojitokeza sasa kwa kuheshimu mipaka ya mihimili, kujua mipaka ya kazi ya utumishi kwa watumishi na viongozi pamoja na kuheshimu Katiba iliyo sheria mama katika nchi. Hakuna aliye juu ya sheria.
Maamuzi ya majukumu ya uongozi na utendaji yafanyike ofisini.
MAGEUZI KWA MFUMO WA JESHI LA PILISI
Kunahitajika jeshi la polisi kufanyiwa maboresho makuwa kwa kuwa na polisi wenye kuwajibika kwa mamlaka ya mahali badala ya jeshi hilo kuwajibika kwa mamlaka ya kitaifa. Hii itapunguza malalamiko yenye kuchukua sura isiyo wazi kwa kutojua mtoa maagizo na yenye kujilia nani ndiye mhusika.
Mamlaka ya kitaifa katika utendaji na maagizo yapitie kwa mamlaka ya mahali ili tukio linalojitokeza lisiwe na utata na kuishia serikali kupata kigugumizi cha kutoa ufafanuzi, lakini maagizo yakipitia kwa kufuata mkondo wa taratibu kuanzia mamlaka za serikali ya itaondoa utata unsojitokeza siku hizi.
Mungu ibarika Afrika
Mungu ibsriki Tanzania 🇹🇿

Upvote
3