BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Rais Joe Biden wa Marekani amekutana na mawaziri wawili wa Ukraine nchini Poland kuonyesha uungaji mkono wa Washington kwa serikali mjini Kyiv wakati Urusi ikiashiria kwamba inaweza kupunguza malengo yake ya kivita nchini Ukraine.
Biden aliketi kwenye meza ndefu nyeupe pamoja na mawaziri wake wa mambo ya nje Antony Blinken na yule wa ulinzi Lloyd Austin na upande wa pili alikuwepo waziri wa mambo ya kigeni wa Ukraine Dmytro Kuleba na waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Oleksii Reznikov.
Kulingana na Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani, mkutano huo kati ya Biden na mawaziri wa mambo ya nchi za nje na ulinzi wa Ukraine ulijikita kwenye kusisitiza dhamira ya Marekani katika kutetea uhuru na hadhi ya mipaka ya Ukraine.
Mazungumzo hayo yamefanyika wakati Urusi imeendelea kufanya mashambulizi kwenye mji wa bandari wa Mariupol kwa kuyalenga makazi ya watu na vituo vya kijeshi kutokea angani na ardhini.
Katika hatua nyingine iliarifiwa jana kuwa vikosi vya Urusi vimechukua udhibiti wa Mji wa Slavutych ambao ni makazi ya wafanyakazi wa kinu cha nyuklia cha Chernobyl.
Putin alituma vikosi vyake nchini Ukraine tangu Februari 24, akiahidi kulisambaratisha jeshi la nchi hiyo na kuuangusha utawala unaoegemea upande wa magharibi wa rais Volodymyr Zelensky.
Source: DW