Rais Biden amteua Karine Jean-Pierre kuwa msemaji mkuu wa Ikuku ya Marekani

Rais Biden amteua Karine Jean-Pierre kuwa msemaji mkuu wa Ikuku ya Marekani

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,483
BIDEN, JEAN-PIERRE WAWEKA REKODI MAREKANI
Rais wa Marekani, Joe Biden amemteua Karine Jean-Pierre kuwa msemaji mkuu wa Serikali kuanzia wiki ijayo.
Karine Jean-Piere anakuwa mwanamke wa kwanza mweusi kushika wadhifa huo katika historia ya Marekani.

Jean-Pierre 44, anachukua nafasi inayoachwa wazi na Jen Psaki anayetajwa kujiunga na kituo cha utangazaji cha MSNBC.

Kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo wa juu wa utoaji habari na majadiliano na waandishi wa habari, Karine Jean-Pierre aliwahi kuwa mnadhimu mkuu wa kambi ya Kamala Harris baada ya Harris kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Joe Biden kwenye uchaguzi mkuu wa Marekani.

Uteuzi wa Karine Jean-Pierre unatajwa kuwa moja ya mkakati wa Rais Biden na makamu wake Kamala Harris kuelekea kwenye uchaguzi mdogo wa katikati ya muhula utakaofanyika mwezi Novemba ambao unatajwa kutoa taswira ya namna rais anayekuwa madarakani atakavyoweza kumaliza kipindi cha muhula wake.

Mbali ya nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika, Karine Jean-Pierre pia alikuwa msemaji mkuu wa shirika la utetezi la MoveOn wakati wa uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2016.

Mtangulizi wake wa nafasi ya msemaji mkuu wa ikulu ya Washington, Jen Psaki amemsifia Jean-Pierre kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika “mwanamke wa kupigiwa mfano” mwenye “maadili ya juu”.

FB_IMG_1651835693509.jpg
 
... hivi inawezekana vipi mtu kuacha kazi ya kuwa msemaji mkuu wa serikali ya Marekani akaenda MSNBC?
 
Kumbe kateuliwa kwa shukra ya kazi kubwa ya kubwabwaja ktk uchaguzi.
Ni walewale tu kama Bongo land kutoa takrima kwa watoto wa wa zee walioongoza nchi.
Wana siasa kote ulimwenguni shetani wao mmoja tu.
 
Anatafuta kiki kwa ma negros...
 
... hivi inawezekana vipi mtu kuacha kazi ya kuwa msemaji mkuu wa serikali ya Marekani akaenda MSNBC?
Ni kazi nzito mno kuwa mseemaji wa raisi ambae akijisemea anasahahu sahua na kuchanganya vitu, Huyu mwafrika nae anaenda kuwa msemaji wa raisi mwenye matatizo kibao ya mental health.
 
BIDEN, JEAN-PIERRE WAWEKA REKODI MAREKANI

Mtangulizi wake wa nafasi ya msemaji mkuu wa ikulu ya Washington, Jen Psaki amemsifia Jean-Pierre kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika “mwanamke wa kupigiwa mfano” mwenye “maadili ya juu”.
Yani maadili ya juu, na mfano wa kuigwa... ktk ndoa za jinsi moja
 
Ni kazi nzito mno kuwa mseemaji wa raisi ambae akijisemea anasahahu sahua na kuchanganya vitu, Huyu mwafrika nae anaenda kuwa msemaji wa raisi mwenye matatizo kibao ya mental health.
ina wezekna ndio maana mwenzie kaona bora akapambane na utangazaji
 
Back
Top Bottom