- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Video hii hapa chini inadai Rais wa Marekani atahamia Zanzibar. Ina ukweli?
Video ya Rais Biden
Video ya Rais Biden
- Tunachokijua
- Joe Biden ni Rais wa 46 wa Marekani aliyeanza kuhudumu mwaka 2021 ambapo mara baada ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika November 2024 uongozi wake kama Rais wa Marekani utakoma.
Kumekuwepo na kipande cha video kinachomuonesha Rais huyo akieleza kuwa mara baada ya kumaliza uongozi wake atahamia Zanzibar yeye na familia yake na tayari ameshanunua eneo huko, video hizo zipo hapa na hapa.
Uhalisia wa video hiyo upoje?
JamiiCheck imefuatilia video hiyo na kubaini kuwa imehaririwa kwa kuwekewa sauti kwa kutumia teknolijia ya akili mnemba (AI). Utafutaji wa kimtandao kupitia Google Reverse Image Search umebaini kuwa kumekuwepo na video inayofanana na hiyo iliyowekwa tarehe 26-07-2022 ambayo inaeleza kuwa Rais Joe Biden ametoa hotuba kwa waliohudhuria Mkutano wa 46 wa Mafunzo na Maonyesho ya Kila Mwaka ya Shirika la Kitaifa la Watendaji Weusi (NOBLE) huko Orlando, Fla.
Aidha JamiiCheck imebaini kuwa video hiyo imetengenezwa na kuhariririwa sauti na Teknolojia ya Akili mnemba (AI) ijulikanayo kama Elontalks ambayo inamuwezesha mtumiaji kuweka maneno ambayo anahitaji yazungumzwe na mtu maarufu anayemuhitaji mfano Joe Biden, Elon Musk, Barack Obama, Donald Trump na wengineo.
Aidha kwenye chanel ya IBJmedia iliyopandisha video hiyo kwenye mtandao wa Youtube tarehe 25-10-2024 kuna maelezo ambayo yanaeleza kuwa sauti ama video hiyo inaweza kuwa imehaririwa ama imetengenezwa kwa njia za kidijitali, haya ni masharti ya mtandao huo kwa watu wanaoweka video zisizo halisi.