Superman, Heri ya Mwaka Mpya!
Umeleta mada nzuri sana, hasa tukielekea uchaguzi mkuu wa 2010 hapo mwakani. Ila nadhani ume-dilute uzito wa mada yako kwa kusema Waziri Mkuu atoke JF. Simaanishi kuwa hawezi kutoka Rais au Waziri Mkuu JF, ila nadhani limitation hizo zinatufanya tutazame humu humu tu ambako watu wengi haiyumkini hatujuani uhalisia wetu! Mfano, wewe au yule waweza kuwa kiongozi mzuri kwasababu labda una/mna mawazo mazuri kisisasa, ila si katika nyanja zingine zinazohusu kiongozi bora kama inavyokubalika katika jamii.
Mnapoendelea kuchambua mada hii na kwa kuzingatia katiba yetu ilivyo, lazima kuangalia mambo yafuatayo:
1. Kiongozi lazima awe na sifa zote kisiasa, kitamaduni na kijamii mfano elimu, integrity,nk;
2. Awe na rekodi ya utendaji bora;
3. Ni LAZIMA tutazame chama chake cha kisiasa, mfano, sera zake. Chama cha siasa kina determine mambo mengi,mfano intergrity yake ikoje, kina uwezo wa kuunda serikali, nk nk.
Nashauri tujimwage bila kujali wanaotajwa wanatoka JF au la. I consider this a very serious discussion.