Rais Dkt. John Magufuli kuwakabidhi Kombe Mabingwa wa VPL Simba SC

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, anatarajia kuwakabidhi Kombe Mabingwa wapya wa ligi kuu Tanzania Bara VPL ,msimu huu wa 2017/2018 Simba SC, katika mchezo wa Simba SC dhidi ya Kagera Sugar siku ya Jumamosi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Rais wa TFF Wallace Karia amesema TFF kwa kutumia Ofisi ya Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa Na Michezo wametuma ombi hilo kwa Mh. Rais na wanaamini itakuwa hivyo.

Ili kuhakikisha mchezo huo ambao Rais Dkt. Magufuli atakuwa mgeni rasmi, wameamua kupunguza viingilio, ambapo kwa mzunguko itakuwa 3000 ili kuwapa nafasi watanzania wengi kuungana na Rais Magufuli.

Aidha, kabla ya kuwakabidhi Kombe Simba SC, Mh. Rais atapokea Kombe kutoka kwa Vijana wa Serengeti Boys U17 ambao walilipata wiki chache katika mashindano ya Challenge yaliyofanyika nchini Burundi.

Kukabidhiwa Kombe na Vijana huo kwa rais ni ishara ya maandalizi ya Tanzania katika mashindano ya Vijana ya AFCON mwaka 2019 ambapo Tananzia itakuwa mwenyeji wa mashindano.



======

UPDATE;

Shirikisho la soka nchini TFF leo Mei 16, limethibitisha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekubali ombi la kuwa mgeni rasmi na kukabidhi vikombe vya ubingwa wa Serengeti Boys na Simba.

Mtendaji mkuu wa TFF Wilfred Kidao amesema wamethibitishiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa Rais Magufuli amekubali kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Simba SC dhidi ya Kagera Sugar jumamosi hii.

''Rais Magufuli amekubali ombi la TFF kuwakabidhi vijana wa Serengeti Boys Kombe la CECAFA waliloshinda hivi karibuni nchini Burundi, tukio ambalo litaambatana pia na kuikabidhi Simba SC kombe la ubingwa wa VPL msimu huu'', amesema.

Serengeti Boys wameibuka mabingwa wa soka katika ukanda wa Africa Mashariki na Kati baada ya kutwaa ubingwa huo kwa kuwafunga vijana wa Somalia kwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali.

Simba imetwaa ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2017/18 baada ya kufikisha alama 68 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kati ya 16 za ligi kuu msimu huu.
 
Hili kombe mwaka huu limewatia uchizi hawa jamaa
Simba SC imepindua meza kibabe kutoka kwa TFF ya Malinzi, safari hii mbona mtaongea Kichina na kutambua kuwa..This is Simba SC
 
Walikuwa na kiu sana kkulipata ss imekuwa kero kama vile wamechukua club bingwa afrika bhan
Mbona kilio sana Vyura FC? Kwani mlivyokuwa nalo hamkujua ipo siku watachukua wengine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…