Nimewawekea mahojiano ya Rais Kikwete na Waandishi nusu saa ya mwanzo hewani. Unaweza kusikiliza kupitia KLH NEWS INTERNATIONAL na angalia kwenye menu yajuu panaposema "Podcasts". Labda itawapa mwanga kwanini sikuweza kuendelea kusikiliza hadi mwisho..!
me nijuavyo baraza hilo liliundwa ki ushkaji tuu sasa ka sie tumekaa busy kusubiri jama avunje ushikaji huoo basi tunajidanganyaaa..sana sana wat he will do ni ku badilishia sehemu za ulaji tuu which wont b kuvunja baraza hilo or kuondoa mawaziri flani
Kweli kabisa, nadhani ndivyo "wafaidika" wa baraza hilo wanavyoiona na wanatamani iendelee kuwa hivyo. Siye kina kuku tunamwomba Mwenyezi Mungu atukubalie dua letu limpate mwewe inshaallah.
Kweli nimesikiliza mahojiano hayo, sikumsikia akitamka kuwa havunji baraza la mawaziri. Alisema waliunda baraza lililopo kutokana na mahitaji, na wataliangalia "mbele ya safari" wakiona kuna haja ya kurekebisha watafanya marekebisho. Sasa mie sijajua kama hapo "mbele ya safari" tushafika ama bado!