Rais Hussein Mwinyi umelisikia hili la KMKM?

Rais Hussein Mwinyi umelisikia hili la KMKM?

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
leo kumezuka tafran katika social media baada ya clip inayozidi kutrend ,ikionyesha askari wa KMKM wakiwapiga risasi wananchi huko katika mikondo ya bahari. Kinachodaiwa ni askari hao kuwataka au kuwanyang'anya matangi ya mafuta wenye maboti ya kuvulia wakati wakivua katika bahari kuu.

Kinachosikika ni wananchi hao wa Chwaka kusema hatuogopi risasi,mwengine akisema risasi zinapigwa juu, wavuzi walikuwa katika uvuvi wa vibua au dagaa, ndio sana uvuvi huu unawakusanya linapoonekana dagaa njingi na huitana kwa kila mmoja kuchota au kupata ukusaji kwa kadiri ya juhudi yake.

Hali hii ni hatari kwa maana sasa askari wanaotegemewa wamekuwa majambazi na kuwavizia wavuvi inatia wasiwasi huwenda wapo ambao vyombo vyao havikurudi na kusemwa wamepotea au kufa baharini kumbe wameuliwa na kupokonywa zana zao na chombo kuzamishwa kupoteza ushahidi. Ila katika kundi la mamba inasemekana na kenge wamo.

Kuna haja ya wahusika wote kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili kurudisha ule msemo wa uchumi wa buluu ambao hata KMKM walionekana kuupigia debe.

Je, haya au huu ndio ule msemo wa Yajayo yanafurahisha?
 
Hao kmkm ndio mgambo wa zenji ama?

Anyway wajitahidi wasimamie vzr..na wanachi waache uvuvi haramu unaharibu madharia ya samaki.


#MaendeleoHayanaChama
 
Wavuzi ndio watu gani huko chukwani

USSR
 
Hawa mgambo wa zenji nao wanataka kuleta taharuki,huko visiwani!!
 
Back
Top Bottom