Rais Hussein Mwinyi: Zanzibar inakabiliwa na ugonjwa wa Corona

bne

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2016
Posts
1,679
Reaction score
2,016
Rais wa Zanzibar leo ametangaza rasmi kuwa Zanzibar inakabiliwa na ugonjwa wa korona na ametaka taadhari za lazima sasa zichukuliwe.

Kauli hii ni ya kwanza kutolewa na kiongozi wa juu wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na pia ni tofauti kabisa na kauli zinazotolewa na Rais Magufuli.

Your browser is not able to display this video.

======

Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Mwinyi akiwa katika ibada ya Ijumaa katika msikiti wa Mfereji wa Wima amedokeza kuhusu kuwapo kwa gonjwa la Corona katika Kisiwa hicho.

Akiongea na Waumini baada ya swala ya ijumaa Dkt. Mwinyi amesema "Ndugu zangu tumekabiliwa na tatizo hili la ugonjwa wa Covid ulioathiri afya lakini pia umeathiri uchumi wa nchi yetu. Lakini Alhamudulillah muelekeo unaonekana ugonjwa huu unapungua na Insha Allah kwa dua zetu sote utakwisha na In Shaa Allah uchumi wetu utarudi katika hali ya kawaida na utaongezeka zaidi."

Zaidi ya hayo, Dkt. Mwinyi ameshukuru Viongozi wa msikiti kumpa nafasi ya kuongea
 
Ni lini mzee alisema hakuna korona? Kwa siku za hivi karibuni? Acheni ushabiki maandazi..nashangaa MTU anakazana kusema hakuna Corona wakati imeshatangazwa tuchukue tahadhari labda mzee awe anakuja kuwavalisha barakoa na kunawa mikono asubuhi na mchana ndio mtaridhika...
 
Wewe acha uwongo, leo msemaji wa serikali amtangaza rasmi kuwa Tanzania imeweza kuidhibiti corona, sasa wewe na msemaji wa serikali nani mkweli
 
Mkuu umeandika haraka kama upo UCHI. Pili Mwinyi sio kiongozi wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, tatu inabid umtafute Honi Sigara ujifunze kiswahili kidogo.
 
Unavyo jitahidi kumtetea huyo Mzee wako, utadhani ana faida yoyote ile!!🤔
 
Zanzibar ni nchi
 
Tupe chanzo cha habari!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…