Mimi bado siamini unachokisema wezetu wanaondokana na kilimo,Hawa jamaa wanalima kwelikweli tena kwa ma large scale kweli kweli tena kwa kilimo cha mimashine mikubwamikubwa.
Kukidharau kilimo ni kujaribu kuidanganya akili na hata hivyo bado nafikiri ni miujiza kwa nchi kuendelea kama chakula chote ni Tegemezi.Hawa watu hawategemei uchumi wao sana ktk kilimo ni kwasababu hali ya hewa yao iko LIMITED,na hata hivyo mda mchache takribani miezi mitano inayowaruhusu kufanya kilimo wanaitumia vilivyo na hata baadae Kutupatia MSAADA tunapokumbwa na njaa.Na kusema hawa jamaa hawalimi mie nafikiri ni PROPAGANDA zisizo na Tija .
Pia naamini HAKUNA Elimu bora,Utawala wa sheria,mfumo bora wa afya,mfumo bora wa kiuchumi n.k sehemu palipo na NJAA.Kwa kufupisha ni kwamba hakuna binadamu mstaraabu aliye na njaa.
Bado naamini ni swala ambalo limekaa ki intuitive zaidi ya kwamba binadamu hawezi kuwa na mipango na mikakati kabla hujashiba ,hivyo kujikombowa kwetu kutakuja nafikiri ni baada ya kwa nchi yetu kutofikiri tena kesho tutakula nini.
Pili maendeleo hayategemei yule kaacha lile ama hili ama kaendelea kwa lile ama lile bali yanakuja kwa kuitumia fursa iliyopo kwa ufasaha zaidi ,Fursa ya kilimo ni moja ya fursa malidadi ambayo inaweza kutukwamuwa kwani tukiweza zalisha chakula kingi nchi zinazotuzunguka zinahitaji zaidi chakula hicho wenda zaidi ya dhahabu ama tanzanite inavyohitajika ulaya.