Rais John Pombe Magufuli na madafu ya Odeon Cinema

Rais John Pombe Magufuli na madafu ya Odeon Cinema

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
1549422609717.png


Ndugu zangu hii clip ya Rais Magufuli akinywa madafu Odeon Cinema imenikumbusha mbali sana.
Kwanza imenikumbusha jengo la senema yenyewe ambayo sisi tumezaliwa tumeikuta na umaarufu wake kwa kuonyesha michezo ya Kihindi ya akina Ranjan na Babrao katika miaka ya 1950 na katika 1960s uwanja ukawa wa Amitabhachan na wenzake.

Pili hayo madafu aliyonunua rais mwenyewe amenikumbusha mshabiki mkubwa wa Sunderland na Simba - Bin Sudi ambae alikuwa muuza madafu mashuhuri hapo Odeon Cinema.

Lakini zaidi mimi nimekulia mitaa hiyo nyuma tu ya Odeon - Libya Street kwa hiyo kwa muda nilikuwa nimerudi nyumbani.

Rais Mwinyi aliondoa katika urais na Ikulu yenyewe ile "mysticism," iliyokuwapo ya kwanza urais wenyewe kutisha na jumba la Ikulu kutia hofu kama jumba la Count Dracula.

Rais Kikwete yeye alipochukua kiti cha urais ndiyo kabisa katika kazi ya urais ikawa imeingia, "flamboyance," haijapatapo kuonekana khasa jinsi mkewe Bi. Salma alivyoibadili Ikulu kwa haiba yake na kila kitu chake.

Ilipendeza sana kuwaona pamoja.

Rais Magufuli kaja na staili nyingine kabisa haijapatapo kuonekana ila kwa ufahamu wangu mahali pamoja Afrika - Misri.

Hii staili ya madafu imeshabihiana sana na staili ya Anwar Sadat akitokea mahali kama Taharir Square, Cairo (mfano wa Mnazi Mmoja) msafara ukasimama rais akasalimiana na wananchi kisha rais akakaribishwa chai na sandwitch na muuza mgahawa wa hapo na rais akakipokea kikombe na sandwitch akakaa kitako na kunywa.

Kama ilivyo Cairo punde sehemu yote ile itakuwa watu wameshajazana kumshuhudia rais anakunywa chai ya mtaani katika genge.

Nilipokuwa naangalia hii clip nikamkumbuka Anwar Sadat.

Hakika Rais Magufuli anatusuuza kwa haya kwani rais anakuwa mtu kama binadamu anavyokuwa.
Rais anakuwa mtu anaezungumza akacheka na kachekeshwa na akaonyesha furaha na kisha kuwafurahisha kwa kupiga duru ya madafu.

Sijui marais wajao watakuwaje...

https://youtu.be/-pJNfG1DnSk
 
..kaka mbona umemsahau Mzee Lowassa alivyokunywa uji maeneo ya kariakoo?

..baadaye POLISI wakamzuia kufanya ziara za kujichanganya na wananchi.

..tatizo ni kwamba "yeye" tu ndiyo anataka aonekane yuko karibu na wananchi.

..wakifanya wenzake wanatimuliwa kama " mbwa koko."
 
Back
Top Bottom