Rais Karume Akagua Gwaride la Idd - Imekaaje?

Allien

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2008
Posts
5,546
Reaction score
1,861
Asalaam Aleykhum Viongozi;

Nimesikia na kuona katika Taarifa ya Habari ya ITV (very briefly) leo usiku Rais Karume amekagua gwaride la Idd. Niliona gadi moja ya vijana wetu wa kazi FFU.

Hii imekaaje?

Naomba mnisaidie kujua mantiki ya Gwaride katika sherehe za kidini.
 
Karume ni Rais wa Zanzibar na ana mamlaka ya kufanya atakavyo Zanzibar ikiwa ni pamoja na kukagua Gwaride.

Kuhusu mantiki ya gwaride katika sherehe za dini, huenda ni ceremonial tu, kwani Karume alialika mabalozi waliokuwepo Zanzibar pia.
 
Kama ni kweli basi hii ina walakini. Kukagua Gwaride siku ya Idd!!!? 😕
Itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania. Au kakagua gwaride siku moja kabla ili kusherehekea uhuru wa Tanganyika? Kama ni hivyo kwanini hakusubiri hadi leo hii siku ya sherehe yenyewe!?
 
Mkuu; Hapa sijakuelewa. Ina maana anaweza kukagua pia Gwaride la Christmas?
 
Kama ni kweli basi hii ina walakini. Kukagua Gwaride siku ya Idd!!!? 😕

Itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania. Au kakagua gwaride siku moja kabla ili kusherehekea uhuru wa Tanganyika? Kama ni hivyo kwanini hakusubiri hadi leo hii siku ya sherehe yenyewe!?

Kiongozi Bubu;

Mtangazaji alieleza very clearly kuwa "Rais Karume pia amekagua Gwaride la Idd" na walionyeshwa pia Mabalozi ambao wapo Zanzibar.

Duu! Hakuna Mwanazuoni yeyote anyefahamu juu ya hili atusaidie maelezo ya kuridhisha?
 
Inasemekana:

1. Asilimia 99 ya watu wa visiwa/nchi ya Zanzibar ni Waislam
2. Wakati wa Ramadhani hairuhusiwi kula/kuuza chakula mchana
3. Utamaduni na sheria za Zanzibar zinaheshimu misingi ya Kiislamu

Kama nilivyosema, inasemekena.
 
Kiongozi;

CIA World Fact Book ya 2008 ina facts hizi juu ya Tanzania:

Population: 40,213,160

Religions:

mainland - Christian 30%, Muslim 35%, indigenous beliefs 35%; Zanzibar - more than 99% Muslim.

Mimi sina uhakika na Souces za Data hizo.

Hata hivyo bado napata tabu ya kujua mantiki ya Gwaride katika sherehe za kidini.
 
Mkuu unahoji visivyohojika. Unauliza visivyoulizwa. Kwenye lugha ya Kiingereza kuna neno 'defacto'. Kwa Kiswahili nadhani neno hilo linamaanisha 'hali fulani inayotambulika kuwa iko hivyo japo siyo rasmi'. Mantiki ya neno hilo imebeba jibu la swali lako.
 
Kiongozi Companero;

Sasa umenichanganya kabisa. Kama huna uhakika na jibu lako bado utakuwa hujanisaidia. Majibu ya "Inasemekana na Defacto" hayatoi jibu kwa swali langu la msingi. My question is very simple and clear. Labda niliweke kwa mapana zaidi.

Kwa kuwa alikagua Gwaride la Idd, je ni kawaida kwa sherehe za Idd kusheherekeshwa na Jeshi la Police?

Na kama Serikali za Tanzania hazina Dini, hii imekaaje?

Na kama ni suala la Defacto, je Gwaride la sherehe nyingine za kidini linaweza pia kuandaliwa?

Katika kuandaa Gwaride, rasilimali watu, muda, pesa na vinginevyo vinatumika na hivyo kuligharimu taifa. Kumbuka Jeshi la Polisi ni sehemu ya Muungano na hivyo hutengewa bajeti n.k.

Sina uhakika kama unanisoma vyema sasa.
 
Mkuu kwa kweli sijui. Ila kwa nchi zinazochanganya dini na siasa sidhani kama hilo ni tatizo. Kwa Kiingereza gwaride linaitwa parade, yaani, kujikusanya na kujionyesha au kuonyesha. Na parade sio lazima liwe la kijeshi. Ni utamaduni tu wa kuenzi kitu, mtu au tukio fulani. sijui Uislamu unasejame kuhusu ku-parade siku ya Idi. Tuwasubiri wanazuoni waje kutuelimisha.
 
Mhe. Dr Karume sio prez wa kwanza kukagua gwaride siku ya sherehe ya Idd. Baada ya Mapinduzi SMZ, imejiwekea taratibu zake katika kusherehekea sikukuu hiyo ikiwa ni pamoja na kuwepo na Baraza la Idd ambapo shughuli mojawapo ni ukaguzi wa gwaride kabla ya hotuba toka kwa kiongozi wa nchi. Ukaguzi wa gwaride hili ni sawa na ule ambao ufanyika katika Mahakama kuu nchini.

Kwa ufupi hakuna la kushangaza hapo...
 
Kiongozi Bubu;

Mtangazaji alieleza very clearly kuwa "Rais Karume pia amekagua Gwaride la Idd" na walionyeshwa pia Mabalozi ambao wapo Zanzibar.

Duu! Hakuna Mwanazuoni yeyote anyefahamu juu ya hili atusaidie maelezo ya kuridhisha?
Siyo kila anachosema Mtangazaji ni sahihi. Hivyo usiwe na tabia ya kuamini kila kitu. Huyo Mtangazaji na chombo chake ITV ni Mabomu. Hakuna kitu kinachoiitwa Gwaride la Idd. Huo ni upotofu. Jaji Mkuu akikagua gwaride kabla ya kuenda kusikiliza kesi hatuiti hilo Gwaride la Korti, au Gwaride la Washtakiwa.Na pia Kama kuna sherehe za Kumsimika Askofu na Mgeni wa Heshima akawa Rais wa Jamhuri(ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu) na akaandaliwa Gwaride la heshima (Guard of Honour) kukagua kabla ya kufanya shughuli ya Kumsimika Askofu. Hiyo ni sahihi. Na gwaride hilo hatuliiti la Kumsimika Askofu.
 
Asante Pakacha;

Naweza nisiamini ninachosikia lakini ninachoona kikawa cha ukweli. Liniona Guard ya FFU ambayo Rais Karume alikagua.

Nashukuru kwa maelezo yenu, ingawa hajakata kiu yangu ya kutaka kujua Mantki yake ni nini. Kama hakuna maelezo, its Ok.
 
Kiongozi Bubu;

Mtangazaji alieleza very clearly kuwa "Rais Karume pia amekagua Gwaride la Idd" na walionyeshwa pia Mabalozi ambao wapo Zanzibar.

Duu! Hakuna Mwanazuoni yeyote anyefahamu juu ya hili atusaidie maelezo ya kuridhisha?

Sioni uhusiano wowote wa sikukuu ya Idd na kukagua gwaride, labda watatoa maelezo zaidi ili kufafanua kwanini gwaride lilikaguliwa siku ya Idd vingivevyo ni miujiza ya viongozi wetu kufanya mambo ambayo hayaingii akilini.
 
Mhe. Dr Karume sio prez wa kwanza kukagua gwaride siku ya sherehe ya Idd. Baada ya Mapinduzi SMZ, imejiwekea taratibu zake katika kusherehekea sikukuu hiyo ikiwa ni pamoja na kuwepo na Baraza la Idd ambapo shughuli mojawapo ni ukaguzi wa gwaride kabla ya hotuba toka kwa kiongozi wa nchi. Ukaguzi wa gwaride hili ni sawa na ule ambao ufanyika katika Mahakama kuu nchini.

Kwa ufupi hakuna la kushangaza hapo...

Ni kiongozi gani mwingine wa SMZ aliyewahi kukagua gwaride siku ya Idd alipokuwa madarakani?
 
How do you say that in English?
Hili swala la Kiingereza naona umelishikia bango kinoma! Anyway I'll write in english when is needed! So far threads zote ninazo changia zipo kwa kiswahili..😀
 
Back
Top Bottom