Asalaam Aleykhum Viongozi;
Nimesikia na kuona katika Taarifa ya Habari ya ITV (very briefly) leo usiku Rais Karume amekagua gwaride la Idd. Niliona gadi moja ya vijana wetu wa kazi FFU.
Hii imekaaje?
Naomba mnisaidie kujua mantiki ya Gwaride katika sherehe za kidini.
Karume ni Rais wa Zanzibar na ana mamlaka ya kufanya atakavyo Zanzibar ikiwa ni pamoja na kukagua Gwaride.
Kuhusu mantiki ya gwaride katika sherehe za dini, huenda ni ceremonial tu, kwani Karume alialika mabalozi waliokuwepo Zanzibar pia.
Kama ni kweli basi hii ina walakini. Kukagua Gwaride siku ya Idd!!!? 😕
Itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania. Au kakagua gwaride siku moja kabla ili kusherehekea uhuru wa Tanganyika? Kama ni hivyo kwanini hakusubiri hadi leo hii siku ya sherehe yenyewe!?
Inasemekana:
1. Asilimia 99 ya watu wa visiwa/nchi ya Zanzibar ni Waislam
2. Wakati wa Ramadhani hairuhusiwi kula/kuuza chakula mchana
3. Utamaduni na sheria za Zanzibar zinaheshimu misingi ya Kiislamu
Kama nilivyosema, inasemekena.
Mkuu unahoji visivyohojika. Unauliza visivyoulizwa. Kwenye lugha ya Kiingereza kuna neno 'defacto'. Kwa Kiswahili nadhani neno hilo linamaanisha 'hali fulani inayotambulika kuwa iko hivyo japo siyo rasmi'. Mantiki ya neno hilo imebeba jibu la swali lako.
Siyo kila anachosema Mtangazaji ni sahihi. Hivyo usiwe na tabia ya kuamini kila kitu. Huyo Mtangazaji na chombo chake ITV ni Mabomu. Hakuna kitu kinachoiitwa Gwaride la Idd. Huo ni upotofu. Jaji Mkuu akikagua gwaride kabla ya kuenda kusikiliza kesi hatuiti hilo Gwaride la Korti, au Gwaride la Washtakiwa.Na pia Kama kuna sherehe za Kumsimika Askofu na Mgeni wa Heshima akawa Rais wa Jamhuri(ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu) na akaandaliwa Gwaride la heshima (Guard of Honour) kukagua kabla ya kufanya shughuli ya Kumsimika Askofu. Hiyo ni sahihi. Na gwaride hilo hatuliiti la Kumsimika Askofu.Kiongozi Bubu;
Mtangazaji alieleza very clearly kuwa "Rais Karume pia amekagua Gwaride la Idd" na walionyeshwa pia Mabalozi ambao wapo Zanzibar.
Duu! Hakuna Mwanazuoni yeyote anyefahamu juu ya hili atusaidie maelezo ya kuridhisha?
Siyo kila anachosema Mtangazaji ni sahihi. Hivyo usiwe na tabia ya kuamini kila kitu. Huyo Mtangazaji na chombo chake ITV ni Mabomu. Hakuna kitu kinachoiitwa Gwaride la Idd. Huo ni upotofu. Jaji Mkuu akikagua gwaride kabla ya kuenda kusikiliza kesi hatuiti hilo Gwaride la Korti, au Gwaride la Washtakiwa.Na pia Kama kuna sherehe za Kumsimika Askofu na Mgeni wa Heshima akawa Rais wa Jamhuri(ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu) na akaandaliwa Gwaride la heshima (Guard of Honour) kukagua kabla ya kufanya shughuli ya Kumsimika Askofu. Hiyo ni sahihi. Na gwaride hilo hatuliiti la Kumsimika Askofu.
Kiongozi Bubu;
Mtangazaji alieleza very clearly kuwa "Rais Karume pia amekagua Gwaride la Idd" na walionyeshwa pia Mabalozi ambao wapo Zanzibar.
Duu! Hakuna Mwanazuoni yeyote anyefahamu juu ya hili atusaidie maelezo ya kuridhisha?
Mhe. Dr Karume sio prez wa kwanza kukagua gwaride siku ya sherehe ya Idd. Baada ya Mapinduzi SMZ, imejiwekea taratibu zake katika kusherehekea sikukuu hiyo ikiwa ni pamoja na kuwepo na Baraza la Idd ambapo shughuli mojawapo ni ukaguzi wa gwaride kabla ya hotuba toka kwa kiongozi wa nchi. Ukaguzi wa gwaride hili ni sawa na ule ambao ufanyika katika Mahakama kuu nchini.
Kwa ufupi hakuna la kushangaza hapo...
Ni kiongozi gani mwingine wa SMZ aliyewahi kukagua gwaride siku ya Idd alipokuwa madarakani?
Sina hakika na Mzee Ruska kwani alishika nafasi ya uprez kwa muda mchache sana
- Komandoo Salmin
- Wakili
- Jumbe
Hili swala la Kiingereza naona umelishikia bango kinoma! Anyway I'll write in english when is needed! So far threads zote ninazo changia zipo kwa kiswahili..😀How do you say that in English?