Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 144
SIKU moja baada ya Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kuwahakikishia wananachi na wageni kuwa Zanzibar ni shuwari na atakayetaka kutembelea anakaribishwa mripuko mkubwa umetokea katika nyumba moja Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mripuko huo umetokea majira ya saa 4 usiku katika nyumba ya Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ramadhan Issa Kipaya Mtaa wa Mtemani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba na kusababisha nyumba hiyo kuharibika eneo la kuta zake lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
Juzi katika ziara yake ya ziku mbili Kisiwani Pemba Rais Amani Karume amewahakikishia wananchi na wageni wanaotaka kutembelea katika visiwa vya Zanzibar kuwa Zanzibar ni shuwari na hakuna matatizo yoyote kama inavyokuzwa na waandishi wa habari kwamba hakukaliki.
Alisema kuwa Zanzibar imekuwa ni nchi ya amani na utulivu tokea miaka ya chuma hivyo mtindo uliojitokeza katika siku za karibuni wa kuchoma moto nyumba hauna maslahi kwa wananchi na badala yake aliwataka wanasiasa waliofilisika kufunga virago na kutafuta shughuli ya kufanya.
Zanzibar kuna amani tena utulivu wa kutosha watu wanafanya shughuli zao za kawaida na tunawalika wengine pia waje kutembelea visiwa hivi na wachane na wale watu wanaosema kuwa Zanzibar hakukaliki, nyumba zaripuliwa hayo ni maneno ya waandishi tu alisema Rais Karume.
Kada huyo anadaiwa kuwa ndio mhamasishaji mkubwa wa wana CCM wenye kuogopa kujitokeza katika uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kisiwani Pemba.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yahya Rashid Bugi alithibitisha kutoka kwa mripuko huo ambao umeshitua kutokana na mlio mkubwa uliotokea katika mtaa huyo ambapo sehemu kubwa ya wananchi wa eneo hilo wlaikuwa majumbani mwao.
Ni kweli mshindo ulikuwa mkubwa sana na watu nyakati hizo walikuwa wamelala na mimi nilikuwa nipo nyumbani naangalia televisheni lakini niliposikia nikatoka na kwenda katika eneo la tukio tukiwa na mkuu wa mkoa wa kaskazini amesema Kamanda Bugi.
Amesema mripuko huo unatokana na bomu linalotengenezwa kwa baruti ambalo hutumika kwa kupasulia miamba baharini na nchi kavu ambapo baadhi ya watengenezaji wa barabara huwa wanatumia kwa kupasulia barabara kubomoa na kuitawanya miamba hiyo.
Haya mabomu hutengenezwa kwa baruti lakini huwa inapasuliwa miamba ya baharini na na nchi kavu pia hutumika hasa kwa wale watengenezaji wa barabara na mlio wake unakuwa mkubwa kama mabomu ya kawaida Alisema Kamanda.
Kamanda Bugi amesema mabomu hayo yaliotokea Mtemani ni sawa na yale yalioripuliwa hivi karibuni katika madaraja ya Piki wilaya ya wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi amesema uripuaji wa mabomu huo anauhusisha na wanachama wa CUF kutokana na kuwa hawataki kuona wananchi wanajitokeza katika uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura unaoendelea Kisiwani Pemba.
Dadi amesema pamoja na kuwa wana uhakika wa wanaoendesha vitendo vya uharamia ni wafuasi wa CUF lakini hawatawachukulia hatua za kuwakamata kwa kuhofia kwenda kuwalisha chakula cha bure ambacho kitaigarimu serikali ya mapinduzi Zanzibar.
Sisi tunawajua wenye kuendesha miripuko na vituko hivi ni hawa CUF lakini hatuwakamati maana hatutaki kuwalisha bure tunataka tukimkamata mtu tumepeleke mahakamani afungwe na sio kumlisha bure amesema Mkuu wa Mkoa Dadi Faki.
Uandikishaji wa daftari la kudumu la wapigakura unaoendelea katika Mikoa mwili Kaskazini Unguja na Kaskazini Pemba umekuwa na matukio ya kila aina huku baadhi yao yakiwa na ya uvunjifu wa amani ambapo jeshi la polisi yatari limeshatoa tahadhari kwa wananchi kutoancha kuwachukulia hatua kali dhidi yao watakaokwenda kinyume na agizo la kudumisha amani katika visiwa hivyo.
SOURCE:ZANZIBAR YETU WEB BLOG.