Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
BALOZI Amina Mohamed ndiye Waziri mpya wa michezo wa Kenya baada ya Rashid Echesa kupigwa kalamu Machi 1, 2019.
Echesa ameangukiwa na shoka katika teuzi za serikali zilizofanywa na Ikulu ya Rais, Ijumaa. Amina, 57, alihudumu katika Wizara ya Masuala ya Kigeni kutoka Aprili 23, 2013 hadi Januari 26, 2018, alipohamishiwa Wizara ya Elimu kabla ya kuteuliwa Ijumaa kuongoza Wizara ya Michezo.
Echesa aliteuliwa kuongoza Wizara ya Michezo mnamo Januari 26, 2018 akisubiri kuhojiwa kabla ya uteuzi huo kuidhinishwa Februari 12 mwaka 2018. Ripoti wakati huo zilienea kwamba Echesa atetemwa.
Hata hivyo, alifaulu kujaza nafasi ya Dkt Hassan Wario. Naibu Rais William Ruto alilazimika kutetea uteuzi wa Echesa alipokuwa na sherehe ya kurejea nyumbani katika eneo bunge la Mumias mnamo Machi 13, 2018.
Echesa alihudumu kama waziri kwa mwaka mmoja kabla ya kutemwa Machi 1, 2019.
Sababu kuu ya Echesa kutaka kutemwa Februari 2018 ilikuwa kutokana na kiwango chake cha chini cha masomo.
βEchesa aliacha kusoma katika darasa la saba,β vyombo vya habari viliripoti Februari 12.
Taifaleo