Rais Kenyatta aonya kuhusu ushindani baina ya China na Marekani barani Afrika

Rais Kenyatta aonya kuhusu ushindani baina ya China na Marekani barani Afrika

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
8,633
Reaction score
16,586
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametahadharisha kuhusiana na ushindani wa Marekani na China barani Afrika na kubainisha kwamba, madola ya kigeni yanazidisha mgawanyiko na mivutano katika bara hilo.

Rais Kenyatta amesema hayo akiwa mjini Washington Marekani na kubainisha kwamba, nchi za Kiafrika zinapaswa kuwa huru katika suala zima la uhusiano na ushirikiano na nchi zote mbili yaani China na Marekani.

Rais Kenyatta amesema kuwa, katika mazungumzo yake ya awali na Rais Donald Trump wa Marekani alionyesha wasiwasi mkubwa alionao wa kurejea katika enzi za vita baridi wakati madola ya Afrika yalipokuwa yakilazimika kuchagua kati ya Marekani na Umoja wa Sovieti.

Rais Uhuru Kenyatta amesema, hatutaki kulazimishwa kuchagua, tunataka kufanya kazi na kushirikiana na kila mtu na tunaamini kwamba, kuna fursa kwa kila mtu.

Rais wa Kenya ameongeza kuwa, madola ya Magharibi na washirika wao wa Asia Magharibi na Asia kwa ujumla yanarejea tena katika ushindani wao barani Afrika ambapo katika baadhi ya mambo madola hayo yanaonekana yakiyapatia silaha baadhi ya makundi na yanafanya mambo kama vile Afrika ni kwa ajili ya kutwaliwa.

China imekuwa ikifadhili miradi ya mabilioni ya dola katika maeneo mbalimbali ya dunia hasa katika sekta ya miundombinu ukiwemo mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kati ya Nairobi na mji wa bandari wa Mombasa.

4bv6a3d82a20e31ld7z_800C450.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
... Good observation by a visionary leader!
 
Bara la Africa ni Kama binti "mrembo" kutokana na rasilimali alizonazo anayegombewa na midume (mabeberu) tofauti tofauti.

Kama huyu Mrembo (Africa) akiwa mjanja anaweza kuangalia jinsi anavyoweza kunufaika kupitia ushindani wa hawa Mabeberu na kufanya maamuzi sahihi.

Muhimu viongozi (watawala) wetu wawe makini na mikataba wanayoingia na haya madola makubwa tusije kugawanywa na kutwaliwa tena kama ilivyokuwa mwaka 1884 huko Berlin.
 
Back
Top Bottom