Rais Kenyatta avunja kanuni, amnyima Naibu wake fursa ya kuhutubia Taifa

Rais Kenyatta avunja kanuni, amnyima Naibu wake fursa ya kuhutubia Taifa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amekataa kumpa fursa Naibu wake kuhutubia taifa katika maadhimisho ya Siku ya Madaraka, Juni Mosi, 2022

Hii ni mara ya kwanza Ruto amekosa kupewa fursa ya kuhutubia taifa tangu Kenyatta alipoingia madarakani mwaka 2013.

Hatua ya Kenyatta imetafsiriwa na raia wa Kenya kama kilele cha tofauti kati ya Ruto na Kenyatta, ambao hivi karibuni hawakukaa meza moja wakati walipokutana katika maombi ya kitaifa.

Wakenya walishuhudia Rais Kenyatta akivunja kanuni na kuanza kuhutubia taifa baada ya kutoa tuzo za kitaifa na kumwalika Rais wa Sierra Leone, Julius Maada Bio.

Kabla ya hapo, Rais Kenyatta aliongoza kikao cha Baraza la Mawaziri akiwa na mke wake Margaret Kenyatta, bila ya kumwalika Ruto.

Katika hicho, Kenyatta ameshukuru Mawaziri wake kwa kushirikiana naye, na kusema alikuwa na imani kwamba ameweka msingi imara kwa viongozi watakaoingia madarakani baada yake.

Kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement, na ambaye ni mgombea wa Rais anayeungwa mkono na Rais Kenyatta, Raila Odinga, pamoja na mgombea wake mwenza, wamehudhuria sherehe za Madaraka.

Hiyo imekuwa sherehe ya mwisho ya kitaifa kwa Rais Kenyatta kabla ya uchaguzi wa Agosti 9, 2022.

Wafuasi wa William Ruto, anayegombea Urais wametaja hatua ya Rais Kenyatta kumuunga mkono Raila Odinga katika uchaguzi wa Urais kuwa ni usaliti.

Chanzo: DW
 
huyu william ruto apambane kivyake akitegemea uhuru amnadi kwa wananchi ili aweze kupata uraisi basi atafeli
 
bita ni bita mura !

hao walishakua maadui so ni Ruto kupambana k’vyake
 
Back
Top Bottom