Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amezindua kikosi cha kwanza nchini humo cha ulinzi wa baharini.
Kikosi hicho kina jukumu la kulinda na kuangalia mipaka ya Kenya baharini dhidi ya miongoni mwa mengi, uvuvi haramu ambao rais Kenyatta ameeleza unaigharimu nchi takriban dola milioni 100 kila mwaka.
Rais Kenyatta amekizindua kikosi hicho karibu na ufukwe wa mji wa pwani Mombasa, ambapo alizindua chombo cha MV Doria, kitakachotumika kwa uangalizi baharini.