Rais Kenyatta kumkatia rufaa mgombea aliyeruhusiwa na Mahakama

Trump2

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
1,553
Reaction score
2,609
images.jpg

Uhuru Kenyatta amesema anakusudia kukata rufaa maamuzi ya Mahakama Kuu ya kumjumuisha Ekuro Aukot katika kinyang’anyiro cha Urais katika uchaguzi wa marudio.

Kupitia kwa Mwanasheria wake Tom Macharia, Rais Kenyatta aliiambia Mahakama kuwa anakusudia kwenda kwenye Mahakama ya Rufaa Jumatatu ijayo.

Hatua hiyo inakuja baada ya maombi katika hukumu ya Mahakama Kuu kumruhusu Dr. Aukot kugombea Urais kutangazwa na Justice John Mativo.

Jumatano, Justice Mativo alisema kuwa Dr. Aukot lazima ajumuishwe kwenye uchaguzi wa marudio ambao umepangwa kufanyika October 26, 2017.

Mahakama ilikwenda mbali zaidi kuieleza Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kurekebisha katika maandalizi yao na kumjumuisha Dr. Aukot kama mgombea.

Rais Kenyatta kumkatia rufaa Mgombea aliyeruhusiwa na Mahakama | TANZANIA CLASSIC
 
Sasa anapinga anataka abaki mwenyewe ili apite bila kupingwa?
 
Mwenyewe nimeshangaa, yaani sasa naamini aliiba kura, anaogopaje hata mgombea. mdogo kiasi hicho?
 
Ungeweka chanzo ili tujue usahihi wa habari yako maana katika hali ya kawaida Kenyata ni yuko madarakani na anategemwa kushinda tena hata kama Raila asingejitoa kwenye uchaguzi. Sina uhakika kama anaweza kupoteza mda wake kwenda kupinga mtu mabae hana madhara kwenye uraisi wake.
 
Mbona kila siku zinavyokwenda Uhuru anajawa hofu na mambo ya ajabu ajabu? Huyu ndo tumuige kweli kuwa ni mwana demokrasia? Nitakuwa wa mwisho
 
Mkuu tulia mbona papara? chanzo kaweka , huoni hiyo link hapo chini?
 
mahakama itakataa rufaa yake na wow! uhuru kashinda uchaguzi wa haki naa kidemokrasia
 
Kama mwanamke aliyeolewa ndoa ya kikristo. Hataki mke mwenza
 
kuna uwezekano huyo jamaa akapita kimchezo mchezo
 
Amemkatia rufaa,inamaana hao wagombea wengine walifungiwa.mkuu
 
Mbona kila siku zinavyokwenda Uhuru anajawa hofu na mambo ya ajabu ajabu? Huyu ndo tumuige kweli kuwa ni mwana demokrasia? Nitakuwa wa mwisho
Tatiz9 linakuja uchaguzi wa awali hakuepo inailazimu tume ya uchaguzi ihairishe uchaguzi ili kumjumuisha kwenye karatasi ya kupigia kura maana hakuemo...shida ndo IPO hapo mahakama ya kenya kazi yake ni kuona uchaguzi wa kenya aidha haufanyiki au unavurugika maana haiingii akilini....wanataka kushindana na kenyatta.
 
Akili yako ndogo
Huyo jamaa asipokatiwa rufaa maana yake ni kuwa uchaguzi utaahirishwa na Tume itatangaza tarehe mpya na makaratasi mapya yatatolewa ikiwa na jina la huyo mgombea.
Hebu niambie gharama ambayo imetumika hadi sasa halafu muahirishe uchaguzi kizembe kizembe
 
Tatiz9 linakuja uchaguzi wa awali hakuepo inailazimu tume ya uchaguzi ihairishe uchaguzi ili kumjumuisha kwenye karatasi ya kupigia kura maana hakuemo...shida ndo IPO hapo mahakama ya kenya kazi yake ni kuona uchaguzi wa kenya aidha haufanyiki au unavurugika maana haiingii akilini....wanataka kushindana na kenyatta.

Mahakama ilisema fresh election IEBC wakalazimisha uwe run of ili wagombea wawe wawili tu ndio maana Ekot akshinda mahakamani.
 
View attachment 607648
Uhuru Kenyatta amesema anakusudia kukata rufaa maamuzi ya Mahakama Kuu ya kumjumuisha Ekuro Aukot katika kinyang’anyiro cha Urais katika uchaguzi wa marudio.

Kupitia kwa Mwanasheria wake Tom Macharia, Rais Kenyatta aliiambia Mahakama kuwa anakusudia kwenda kwenye Mahakama ya Rufaa Jumatatu ijayo.

Hatua hiyo inakuja baada ya maombi katika hukumu ya Mahakama Kuu kumruhusu Dr. Aukot kugombea Urais kutangazwa na Justice John Mativo.

Jumatano, Justice Mativo alisema kuwa Dr. Aukot lazima ajumuishwe kwenye uchaguzi wa marudio ambao umepangwa kufanyika October 26, 2017.

Mahakama ilikwenda mbali zaidi kuieleza Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kurekebisha katika maandalizi yao na kumjumuisha Dr. Aukot kama mgombea.

Rais Kenyatta kumkatia rufaa Mgombea aliyeruhusiwa na Mahakama | TANZANIA CLASSIC
hiii ni muharo news
 
Mwenyewe nimeshangaa, yaani sasa naamini aliiba kura, anaogopaje hata mgombea. mdogo kiasi hicho?
Probably anaangalia ile 12b imekabidhiwa iebc kuandaa uchaguzi ujao..it's not rocket science
 
Back
Top Bottom