Wandugu ndio uongozi huo......juzi tu alikuwa anapiga misele mikoani kwenye vumbi ili wadanganyika muache kidomodomo; sasa anaenda kupata 'bubble bath' na mai waifu wake mamtoni. Sisi tutaendelea kumshikia nchi yake tu pindi awapo safarini. Akirudi libeneke kama kawa....kwikwikwi!!
Nani anasema alikwenda mikoani kwa manufaa ya watanzania?
Mwenzenu alikua keshaanza kampeni kisirisiri kabla hata wenzake wapinzani hawajui, ili aongezewe muda wa kula.
Kama alikwenda mikoani kuangalia miradi iliyowekwa na serikali inaendeleje kwanini anawauliza watu wa Mombo kwamba shida zenu ninini?
Kuna diwani wa serikali
Mbunge wa serikali
Diwani anapeleka shida za wananchi kwa mbunge
Mbunge anapeleka shida bungeni zipatiwe ufumbuzi
Mtu yeyote aniambie kama kuna diwani na mbunge kwanini aje kuulizia wananchi shida za Mombo?
Halafu watu mnalalamika eti watu hawaandamani lakini watanzania wengi wameamka sasa.
Juzi nilikua Mombo pale kuelekea Lushoto tukasimamishwa eti msafara wa mheshimiwa unataka kupita. Mheshimiwa alipokua anakwenda Lushoto wengi waliokuja kumlaki walikua watoto wa sekondari na msingi.
Jamaa anayekusanya alikua anawatafuta watu anasema jamani kusanyikeni kwa wengi akiona tuko wengi atasimama, wapi kila mtu anaendelea na shughuli zake.
Bwahaaaaa na kile kidiwani cha Mombo bomu kabisa, kimeulizwa maswali na JK kinatetemeka na wala hata hakijui shida za watu wake.
Sasa fikiria diwani wa CCM hajui shida za wananchi wake
Mbunge wa CCM hajui shida za wananchi wake, nilipopeleleza nasikia huyo Mbunge wa jimbo lile toka apate chake mapema [kura] hajawahi kufika Mombo
Kiujumla safari ya Tanga ilikua balaa kwake,
Alitaka kwenda Pangani kufika kwenye kivuko kimeharibika
Wananchi wakamuambia ndugu mheshimiwa mbali ya kwamba maisha ni magumu lakini hata hiki kivuko chetu kwa mamiaka sasa hakina ufumbuzi.
Wanachi wengi wa Pangani walifurahi kwamba mhe kuliona hilo na wengine walikasirika kwamba angepata kuvuka ili aje kuona na shida nyingine huku ng'ambo.
Tanzanians we have a long way to go