Rais Kikwete aenda Marekani


Mkuu una haki ya kuandika kile ambacho unaamini. Hoja ya msingi inayofanya wananchi wengi isipokuwa wewe pengine kuhoji utendaji wa mkwere ni namna anavyoshindwa kusimamia na kushughulikia kero nzito zinazoididimiza kaya hii lakini kutwa akisafiri huko na kule safari ambazo zinaigharimu serikali yetu fedha nyingi. Umewahi kufikiria kwamba msafara wake unasheheni watu wangapi na kiasi gani cha pesa kinatumika? unafahamu ni zahanati ngapi zingejengwa kwa kutumia pesa hizo? unafahamu kwamba GW Bush amemualika jamaa kwasababu anajua JK ni mpenzi wa safari? Lakini kikubwa unafahamu namna wananchi walalahoi wanavyobugudhiwa kuchangia ujenzi wa madarasa huku hao wakubwa unaowatetea wakila safari zinazoigharimu nchi?

Tuwe wakweli wa nafsi na roho zetu JK anatakiwa ajisahihishe sana katika miaka miwili iliyobaki kuweza kustand chance ya kupata hata 55% ya kura mwaka 2010 kama mbinu za medani hazitotumika!(level playing field)

JF si mtandao wa mtu mwenye malengo ya 2010 hata kidogo,ila ni mtandao uliosheheni wazalendo wa kweli wa nchi ambao hawako tayari kuita shoka jembe! at JF we call a spade a spade!
 
Ameshafika. Atakuwepo mpaka jumamosi August 30.
 
Baada ya uhusiano wa karibu na Uingereza, Israeli, nadhani Tanzania ni ya TATU sasa!
Nini kinaendelea hapa? hatuna mafuta, hatumo kwenye ukanda wa UGAIDI au tunayo URANIUM?
Nina imani tunachebwachebwa kuhusiana na lile dili la AFRICOM. Tusipokuwa macho na kuuliza right questions, pengine tunaweza kuuvaa mkenge. Au ni mimi tu?
 
Ninamtakia Mh. Rais wetu mpendwa safari njema na arejee salama nyumbani.

Ninaelewa majukumu ya kuongoza nchi na AU ni makubwa unahitaji kuwasiliana na marais wenzako katika nchi mbalimbali ili muweze kuzungumzia masuala makubwa yanayohusu watanzania na waafrika.

Mwisho ninamtakia Mh. Rais na ujumbe wake makazi mema hapo USA.
 

Huwa nakagua mafile kwenye Air Force One Yake Mkuu Maana Mengine Mai Waifu Wake Huwa Anambebea Kwenye Kipima Joto Chake!
 
Ni mikoa mingapi ambayo imepata faraja ya kutembelewa na Mheshimiwa Raisi Kikwete na ni mingapi haijaona hata gari yake kukatiza Mkoani kwao ,Je wasiotembelewa na Raisi wanayo haki ya kudai kama kule Tarime na Pemba.

Sasa ni miaka mitatu inakaribia ,sielewe kwa nini hajazunguruka kila Mkoa angalau mara mbili au Tatu ,wakati miaka hiyo ikikatika tayari Raisi ameshafanya ziara ya Marekani mara sita ,safari ambazo zinaigharimu Tanzania mapesa mengi ,japo kwao ni vijisenti.

Hotuba za kila mwezi anazozitoa ni sawa na hotuba ambazo Raisi wa Zanzibar Karume aliwaekea tape waandishi wa habari ili wamsikilize ,kitu ambacho kiliwawacha hoi waandishi hao waliohudhuria kwa kuonyeshwa kali ya mwaka.
Ikiwa inakaribia mwisho wa Mwezi inawezekana sasa mtindo utakuwa ule ule wa Karume kuwekewa tape na kumsikiliza Mh.Kikwete ,wakati yeye akikata mbuga.
 
Mkuu kwani JK akitembelea hiyo mikoa what will those people gain?Na huko ambako so far ameenda ameshawasaidia nini?Isitoshe anaenda kule ambako anajua yeye mwenyewe atapata kitu.
Incase you forgot hii ni nchi ya kitu kidogo na watu wadogo!
 
Rais wetu anakwenda kwenye vitu kama hivi atakapokuwa Marekani.

The Minister for Natural Resources & Tourism
of The United Republic of Tanzania,
The Hon. Shamsa Selengia Mwangunga, MP
Cordially invites you to a
TANZANIA FESTIVE EVENING
In Honor of
H.E. Jakaya Mrisho Kikwete,
The President of the United Republic of Tanzania
To announce the launch of Phase II of
The Tanzania Tourism Advertising Campaign
“TANZANIA THE LAND OF KILIMANJARO, ZANZIBAR AND THE SERENGETI”
CNN-USA
WABC-TV New York
and
To present the 2008 Tanzania Tourism Board Awards
Tuesday, September 23, 2008
6:30 – 9:30 PM
Twenty Four Fifth Ballroom
24 Fifth Ave, (at 9th St)
New York, NY

na hii

 

Attachments

  • image003.gif
    19.3 KB · Views: 69
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…