Rais Kikwete afuata Lissu kumkosoa Nyerere

Rais Kikwete afuata Lissu kumkosoa Nyerere

Bwana Mapesa

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
2,551
Reaction score
1,777
Habari Wakuu?

Kwanza kabla ya yote napenda kutoa chuki zangu za dhati kwa Raisi Kikwete kutokana na hotuba yake mbovu mbovu aliyoitoa juu ya Sakata la Escrow.

Binafsi nimeona matundu mengi " Loop Holes" kwenye hotuba hilo ila hapa nimejikita kwenye maelezo ya kikwete wakati analitolea uamuzi Azimio la kwanza la bunge juu ya Sakata la Escrow.Azimio hilo lili someka kama ifuatavyo;

“Serikali iangalie uwezekano wa kuchukua mitambo ya kufua umeme ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO kwa mujibu wa Sheria za nchi.


Katika kulitolea ufafanuzi Mheshimiwa Prof. Dr. Kikwete alisema yafuatayo..namnukuu

“Pendekezo tumelipokea, ni jambo linalowezekana kufanya. Hata hivyo, tunapopima ujumbe tunaoupeleka kwa jumuiya ya wawekezaji tunachelea kuwa inaweza kuleta hofu na kuwatisha wawekezaji waliopo na wajao. Nalisema hivyo kwa sababu sisi tuna historia ya kutaifisha mali za kamapuni binafsi. Hofu hiyo bado ipo. Tukichukua mitambo hii tunaweza kurudisha hofu za kurudi tulikokuwa na kukimbiza mitaji tunayohitaji kwa uchumi kukua na nchi kupata maendeleo. Nashauri tuendelee kuyapatia ufumbuzi matatizo ya IPTL kila tunapoyabaini. Aidha, Mahakama imetusaidia sana kwa kuamuru mitambo ya IPTL ibadilishwe ili itumie gesi asilia na kutoza bei ya umeme isiyozidi senti nane za Marekani. Tuyafuatiliye haya kwanza.”

Maana ya majibu ya Kikwete hapo juu ni kwamba Mwalimu Nyerere alikosea kutaifisha mali za makampuni binafsi na watu binafsi kipindi cha utekelezaji wa siasa ya ujamaa na kujitegemea.Na kwamba Mwalimu aliwaonea wawekezaji binafsi kwa kutaifisha mali zao.Hivyo kutaifisha mitambo ya IPTL tutarudisha hofu za kurudi tulipokuwa(ENZI ZA NYERERE).Hapa ni dhahiri Kikwete amethibitisha kwamba nyerere alikosea na Tanzania ya sasa haiitaji kiongozi mwenye maamuzi kama ya Nyerere.

KIKWETE kwa taarifa yako, utaifishaji alioufanya Nyerere ulitokana na machungu yake juu ya mali za umma na hiyo baada ya kunusa harufu ya rushwa ndani ya Nyumba yake (Tanzania) akaona njia mbadala ni kusafisha nyumba yake.Sio kiongozi kama wewe ambaye unasubir "TUMBIRI" Kafulila aje kuitikisa nyumba yako to this extent..SHAME ON YOU..

KIKWETE kwa taarifa yako
,
Tanzania haiitaji wawekezaji wabadhirifu na wezi kama Sigh, Ruge, Kagoda, Meremeta,Dowans, richmond na hao wawekezaji watakao ogopa kuja nchini kwa kuogopa kutaifishwa mali zao basi nao si watu safi bali ni wezi..Kwa maana muwekezaji safi kamwe hawezi kuwa na hofu ya kutaifishwa...again SHAME ON YOU...

KIKWETE kwa taarifa yako,wawekezaji wezi kama Sigh ndo wanaowafukuza wawekezaji safi kutokana na wateule wako corrupt ku prefer deals kutoka kwa corrupt investors na kuondoa ushindani wa kiukweli.

Hivyo basi natoa Rai kwa waliomzomea Lissu kwa kumkosoa Nyerere Bungeni wamzomee na Kikwete.Lakin hapa pia unaona utofauti wa akili ya Kikwete na Lissu.Lissu kamkosoa baba ajili ya kutetea taifa, Kikwete umemkosoa Baba kwa ajili ya kutetea wezi.

Wasalaam

naomba kuwasilisha
 
Tukipata ujasiri wakuyasema haya hadharani taif a litapona naugonjwa waakina kikwete maramoja tujipange kuyasema haya ktk tasisi makundi ya vjn nk. Naishia hapo kwass
 
Kwa taharifa yake shame upon him kwa kukandamiza wananchi wake .
 
Back
Top Bottom