Rais kikwete aingilia kati kodi za line.....amezitaka mamlaka husika zikutane haraka ili tatizo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
RAIS KIKWETE AINGILIA KATI KODI ZA LINE.....AMEZITAKA MAMLAKA HUSIKA ZIKUTANE HARAKA ILI TATIZO LIISHE





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameagiza Wizara za Serikali zinahusika na kodi na mawasiliano pamoja na makampuni ya simu za mikononi nchini kukutana mara moja kutafuta jinsi gani ya kumaliza mvutano wa kodi mpya ya kadi za simu hizo za mikononi.

Rais kikwete ametoa maelekezo hayo jioni ya leo, Jumanne, Julai 23, 2013 wakati alipokutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa makampuni ya simu ya TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel katika kikao cha pamoja kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Rais Kikwete amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo wa pamoja kati ya Wizara hizo za Serikali na makampuni ya simu yawe ya kupendekeza jinsi gani ya kuziba pengo la Sh. Bilioni 178 ambazo zitapotea katika Bajeti iwapo kodi hiyo kwa kadi za kuongelea za simu za mikononi italazimika kufutwa na Serikali kupitia marekebisho kwenye Muswada wa Fedha wa Bajeti ya Mwaka 2013/2014.

Rais Kikwete amewaambia wawakilishi wa pande hizo mbili kuwa huwezi tena kuifuta moja kwa moja kodi hiyo bila kutafuta njia nyingine za kupata fedha za kujaza pengo hilo la Sh. Bilioni 178 ambazo tayari Bunge limezipangia matumizi.

"Nawaombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tunaweza kujaza pengo hili la Sh. Bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu,"Rais Kikwete amewaambia wawakilisho hao.

Katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/2014, Serikali imeweka kodi ya Sh. 1,000/= kwa mwezi kwa kila mtumiaji simu kwa ajili ya kufanya mawasiliano kwa kutumia simu ya mkononi.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.





23 Julai, 2013



RAIS KIKWETE AINGILIA KATI KODI ZA LINE.....AMEZITAKA MAMLAKA HUSIKA ZIKUTANE HARAKA ILI TATIZO LIISHE - MPEKUZI HURU

MSHAHARA WA KIMA CHA CHINI KWA M-TANZANIA KWA KILA SIKU HAUZIDI ZAIDI YA NUSU DOLLAR YA KIMAREKANI. KODI YA LINE YA SIMU YA SERIKALI INAIZIDI MSHAHARA WA KIMA CHA CHINI CHA M-TANZANIA AHHH? TANZANIA KWELI KUNA WATU WANAOSHUGHULIKIA MAMBO YA UCHUMI KWELI? KUNA WASOMI WA UCHUMI NCHINI TANZANIA KWELI?
 
...Nilidhani ametoa Amri Kodi hiyo Kufutwa mara moja halafu wao waendelee kuumiza Vichwa kutafuta namna ya Kuziba Pengo hilo, Kumbe ni kinyume Chake, Kwamba Hawezi kuifuta Kodi Hiyo hadi Wapate Njia kwanza ya Kuziba Pengo Iwapo Kodi Hiyo Itaendelea!! Hakuna Jipya.
 

Mobile Operators Association of Tanzania (MOAT) ndio wanaambiwa hayo, read between the lines, kwa kuwa wao ndio walioshawishi, sasa nilazime itoke kwao.
 
Huyu ni Rais msikivu zaidi katika historia tangu tupate Uhuru! Mungu atupe Rais mwenye sifa kama za Kikwete
 
Mobile Operators Association of Tanzania (MOAT) ndio wanaambiwa hayo, read between the lines, kwa kuwa wao ndio walioshawishi, sasa nilazime itoke kwao.

...Si lazima Kila Kauli Uitafutie 'between Lines' yake hata kama hakuna Ulazima Huo. Wakati mwingine unahitaji Common Sense tu.

Kama Raisi ameona kuwa Kodi inayozungumziwa Inawaumiza Wananchi wake anaweza, Kwa mamlaka Tuliyompa, Kuamua Kuisimamisha Kodi husika Kwanza na kuwataka Wahusika kutafuta Njia nyingine ya Kuziba Pengo litakaloachwa na kuondolewa kwa kodi Husika.

Anapowataka Wahusika,MOAT or Whatever, Kutafuta kwanza Njia za Kuziba pengo huku Kodi husika Ikiendelea Kubamiza Wananchi unadhani MOAT whatever watakuja na Jibu kesho au kesho kutwa or Mwaka huu??
It is just Business as Usual, Hakuna Jipya. Too bad that You dont see it That way,Dear.

:yo:
 
Mobile Operators Association of Tanzania (MOAT) ndio wanaambiwa hayo, read between the lines, kwa kuwa wao ndio walioshawishi, sasa nilazime itoke kwao.

Kumbe siku hizi MOAT wanao uwezo wa kutunga na kusaini sheria mpya ya ukusanyaji kodi nchini. Hii ni habari mpya. Hongereni MOAT kwa majukumu mapya mliyopewa japo. Mhhh...Kweli Wadanganyika tunadanganywa kupita kiasi.
 
Kumbe siku hizi MOAT wanao uwezo wa kutunga na kusaini sheria mpya ya ukusanyaji kodi nchini. Hii ni habari mpya. Hongereni MOAT kwa majukumu mapya mliyopewa japo. Mhhh...Kweli Wadanganyika tunadanganywa kupita kiasi.

Hata huelewi kinachoongelewa. MOAT walishawishi watu waipinge hiyo kodi, husomi habari zinazoendelea kwenye Taifa lako? Toka lini MOAT wakatunga sheria za kodi? Unanshangaza!
 

Rais Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete hakurupuki wala hasusi. Kumbuka hilo.
 
Huu ni upuuzi tu, hapa kapendekeza mafisadi wakutane ili wajadili watutoze kiasi gani badala ya 1000, ilibidi kama rais afute kabisa hii kodi ya kijinga isiyo na maana kwa mtanzania.
 


mimi nilijua ni upepo wa siasa tu........jk bana full drama

kweli hili nalo limewakaa pabaya........

wananchi wangechuna dhidi ya upuuzi huu...hakika mwana haramu bila shaka angepita kimya kimya
 
inamaana hizo 178Bil serikali na wanauchumi wake wamekosa kabisa namna ya kuzipata hadi walazimishie kwenye kodi za simu? kweli tuna wanauchumi uchwara...hebu kwa harakaharaka tuzitafute huku


1.TANAPA+KINAPA+NCAA = hawa wakibana mianya ya ufisadi mwingi tutapata zaidi ya Bil 20
2.Migodini = tax incentives zikipunguzwa huku tutapaza zaidi ya bil 110
3. Busines NGOs' = huku tukifungua macho kuna NGO nyingi sana zinafunguliwa na zinajifanya kutoa misaada lakini kiukweli ni business NGO wapigwe kodi hwa tutapata zaidi ya mil 800
4. Mafisadi wabanwe warudishe pesa zote wanazokwapua huku tutapata zaidi ya bil 47.2


kwa hiyo tayari bil 178 tutakuwa nazo hata bila ya kutembeza bakuli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…