mwalimu Jr.
Member
- Aug 20, 2008
- 51
- 4
BILA kutegemewa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye majira ya kama saa tisa hivi aliingia katika Kanisa Katoliki Msasani kuja muaga aliyekuwa mbunge wa Mbeya vijijini, Marehemu Richard Nyaulawa.
Kanisa hapo palifurika mawaziri, wabunge, wanasiasa wa vyama vyote, wahariri wa habari, wastaafu wa serikali kadhaa na kizazi cha waandishi wa habari na wafanyakazi katika vyombo vya habari wanawake kwa wanaume, Wakiristo kwa Waislamu bega kwa bega wakitoa heshima zao za mwisho.
Fundisho nililoona kwa upande wangu kanisani hapo-nje nda ndani ni kwamba hatuna sababu ya kuzusha vigomvi vya kijinga kati ya waumini wetu mbalimbali maana hawa wanaishi pamoja, wanafanya kazi pamoja, wanahudhuria harusi za kila mmoja wao na mwisho wa yote wanazikana.
Marehemu Nyaulawa anasafirishwa kesho Alhamisi kwenda kuzikwa kijijini na nyumbani kwake pale Inyala kando ya jiji la Mbeya.
Richard Nyaulawa na mwenzake Rashidi Mbuguni watakumbukwa kama ndio wazazi wa kizazi cha waandishi wa habari na wafanyakazi katika vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini. wao ndio waliokuwa wa kwanza kuanzisha gazeti binafsi la Business Times ambalo liliendeshwa kama kampuni na sio shughuli au biashara ya nyumbani.
Mungu amlaze mahala pema peponi!