Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ameipongeza Ofisi ya Ukaguzi ya Taifa, NAO, kwa kazi nzuri inayofanya ya kutoa ripoti ya ukaguzi kwa wakati, hivyo kusisitiza ripoti hizo lazima zifanyiwe kazi kwa makini.
Pia Rais Kikwete amesisitiza imani yake kwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, CAG bwana Ludovick Utouh, na kusisitiza kutokana na umuhimu wa ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, hata yeye kama rais wanchi, anayo mamlaka ya kumteua tuu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu lakini hana mamlaka ya kumfuta kazi.
Rais Kikwete alitoa hakikisho hilo, katika hafla fupi ya kupokea taarifa ya Mipango Mkakati ya Mika 3 ya Ofisi ya Ukaguzi ya Taifa, iliyosomwa kwake na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh, kwenye jingo jipya la Ofisi ya Ukaguzi wa Taifa mjini Singida, hivi karibuni.
Rais Kikwete amesema Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, iko kwa mujibu wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyotajwa kwenye ibara ya 144 ya katiba Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, hivyo mamlaka yake kama rais ni kumteua tuu mdhibiti
Nae Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh, akieleza kuhusu mpango mkakati wa miaka mitatu 2008/2011, amesema ofisi yake itaboresha zaidi huduma zake ikiwa ni pamoja na kujidhatiti zaidi katika ukaguzi wa value for money.
Baadhi ya vipengele vya Mpango Mkakati wa Miaka 3 wa Ofisi ya Ukaguzi wa Taifa pamoja na umuhimu wa ofisi hiyo kutakiwa iwe na uhuru zaidi ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Bwano Utouh ametolea mfano wakaguzi kufadhiliwa ofisi na vitendea kazi na mkaguliwa unategemea nini zaidi ya kujisikia kuwajibika kulipa fadhila.
Kauli ya rais kuwaweza kuwateu baadhi ya watendani lakini hana mamlaka, inajibu baadhi ya dukuduku za mgawanyo wa madaraka kati ya vyombo vikuu vitatu vya dola, Bunge, Serikali na Mahakama ambapo kila kimoja kinatakiwa kutimiza majukumu yake kwa uhuru bila kuingiliwa na kingine.
Hivi karibuni, kumeibuka mvutano wa maingiliano kati ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania likiishinikiza serikali kuwachukulia hatua baadhi ya maofisa wake, na serikali kushikilia msimamo wa kiserikali ambapo Bunge halikuridhika.
Ofisi nyingine zinazotajwa na Katiba ambazo rais anayo mamlaka ya kuteua tuu na sio kufukuza kazi ni pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu.