Ni kweli the buck may stop at JK. Kwa mazingira ya Tanzania kuna tatizo la kisheria na utaratibu. Hebu nitoe mfano. Mfumo wa nchi yetu wa the public service delivery system unategemea umahiri na uweledi wa watendaji wa Halmashauri ya Wilaya/Mji/Jiji/Manispaa. Ideally rasilmali pesa, rasilimali watu na kadhalika vinapelekwa kwenye Halmashauri kutoka Serikali Kuu (Central Government) kupitia bajeti ya kila mwaka wa fedha. Hizi ndizo zinatumiwa na sekta mbalimbali kama vile afya, maji,barabara n.k. Afisa Mtendaji Mkuu ni Mkurugenzi ambaye ndiye msimamizi wa matumizi ya mafedha na rasilimali za halmashauri. Kama utendaji wake hauridhishi anayepaswa kuwa jicho la Rais katika ngazi hiyo ni Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa. Huyu DC ndiye anaetakiwa kumkabili huyo Mkurugenzi kwa kumwajibisha na kama anakuwa mbishi na mkaidi basi anapeleka taarifa kwa Mkuu wa Mkoa kuwa mambo pale kwenye Halmashauri yake hayaendi iapsavyo. Nae RC atambana Mkurugenzi. Akikaidi basi anamripoti Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambayo iko ofisi ya Waziri Mkuu. Sasa pale ndipo watamchukulia hatua za kinidhamu dhidi ya huyo Mkurugenzi. Jamani hiyo ndiyo ideally yaani kinadharia.
Hatua atakazochukua TAMISEMI dhidi ya Mkurugenzi zimewekewa taratibu na kanuni za kisheria ambazo Waziri wa TAMISEMI akisaidiwa na Katibu Mkuu wake anapaswa kuzizingatia. La sivyo asipozizingatia Mkurugenzi akienda Mhakamani Waziri anaweza kujikuta anashindwa. Utaratibu huu umeigharimu sana taifa hili kwa sababu imebidi tubakie na watendaji wabovu. Sana sana kuwafukuza ni ngumu kwa sababu wanalindwa na hizi kanuni kwa hiyo anaweza akapewa kazi nyingine. Maana huo uoza unaendelea kuathiri sekta nyingine ya serikali.
Sasa nije kwenye mada. Hapo Rais anaweza kufanya nini. In theory, kwa sababu anavyo vyanzo vingine vya kumpatia taarifa kama vile Usalama wa Taifa, wananchi wa kawaida, magazeti anaweza kuchukua hatua. Lakini kumbuka huyu Rais anayo miaka mitano ya kutekeleza Ilani yake. Kwa hiyo anayo monitoring system ambayo inaangalia utekelezaji. Je reality ikoje?
1. Asilimia kubwa ya bajeti inategemea wafadhili. Mpaka pesa ije na haiji yote unakuta na miezi nayo inayoyoma. Hii inaathiri performance ya serikali.
2. Asilimia kubwa ya watendaji wetu ni mediocre. Why? Wengi wao elimu zao zinatokana na mfumo wa elimu mbovu wa kipindi cha awamu ya kwanza hadi ya tatu. What we sowed in our education system is what we reaping now in what we see as mediocre performance ya serikali.
3. Watendaji wengi wana mahusiano ya kindugu tena ya karibu na wakubwa wa sasa na wawaliopita awamu zilizotangulia ambao ni watoto wao wa kuzaa au wa ndugu zao au mashemeji zao. Na hawa wamo katika idara nyingi tu za serikali kama vile polisi, magereza, idara ya usalama wa taifa, TRA, BOT, Wizarani ndiyo usiseme. Namjua Mkurugenzi mmoja ambaye anaye girlfriend ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara mojawapo serikalini. Sasa katika hali hii unafikiri wabovu hawa hata ukiwachukulia hatua kali wakati system nzima imejaa hao hao unafikiri it can work.
Mimi nasema hata JK na CCM watoeni kwenye madaraka waje CHADEMA hakuna lolote watakalofanya. Kwa sababu we will just have a change of the political leadership and not the Civil (Public) Service System. Sawa CHADEMA itabadilisha Makatibu Wakuu, Wakurugenzi wa Wizara na kadhalika. Lakini unafikiri itawatoa kutoka wapi kama siyo kwenye kundi hili hili bovu. Na watakapokuwa wanatawala wakiona mambo hayaendi kama ilivyokuwa kwa CCM wataanza na wao visingizio unajua hii ni kutokana na miaka mingi ya ukiritimba wa CCM tupeni muda wannchi. Awamu ya Tano ya Sita mpaka milele. Hali ni hiyo hiyo. Tujifunze kutoka Zambia, Malawi. Kwa hiyo wao CHADEMA wachukue serikali halafu tutakuwa na CCM ile ile in style and rhetoric but different attire.