Rais Kikwete anafanya biashara hii?Au utapeli wa DECI umerudi tena?Wakuu tusaidiane.

Rais Kikwete anafanya biashara hii?Au utapeli wa DECI umerudi tena?Wakuu tusaidiane.

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
1,959
Reaction score
876
Wana JF salamu.
Nimepata taarifa hizi za Rais Kikwete kusaidia maskini wa Tanzania kwa kuwapatia mikopo rahisi isiyo na riba tena akishirikiana na Rais Obama.Lakini cha ajabu ni kuwa familia ya Rais ndiyo inayosimamia kwa ukaribu.Lakini pia serikali ndiyo inayofanya kazi hii kwa kushirikiana na benki kuu.Waziri mkuu Pinda ndiye mtendaji mkuu.Jamani inawezekana kweli habari hii au ndio mchezo wa DECI umerudi tena?

Soma habari hii ambayo source yake ni kwenye link hii http:/tanzanialoan.wapka.mobi/index.xhtml


5530326_e70748134f.gif
5530323_752fa78a0d.jpg

5530492_6948f6bcc9.png
5530493_97f6e97bca.jpg
5636955_10d13b03df.gif

Tanzania Loans Society ni tawi zawa la Shirika kubwa nchini marekani liitwalo Advolticies Power Loans Society (APL Society) linalo'ongozwa na Rais Barack Obama. Tanzania Loans Society ni tawi ambalo limeanzishwa mwaka 2012 kwa dhumuni la kutaka kuwasaidia watanzania ambao wanahali duni (masikini) kwa kumuwezesha kumpatia kila mtanzania mkopo wa fedha na zawadi ya Tshs.300,000 bure kwa kila mtanzania atakaejiunga na kua mwanachama wa Tawi hili.

Tawi hili lilianzishwa nchini Tanzania baada ya Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania alipokua katika ziara yake nchini marekani alipata fursa ya kuonana na Rais Barack Obama ndipo alipopewa muongozo na mchanganuo wa shirika la kuwasaidia wamarekani (APL Society) wasiokua na uwezo wa kifedha. Rais Barack Obama alikua na moyo thabit wa kuonesha kujali na akawa tayari kumsaidia Rais Jakaya Kikwete dhidi ya wananchi wake masikini akamshauri kikwete afungue tawi dogo ambalo litakua ni sehemu moja wapo ya shirika la APL SOCIETY ili kuwasaidia watanzania kupata fedha za mikopo.

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho kikwete alikubaliana na shauri hilo la Rais Barack Obama na kukubali kuanzisha tawi zawa la APL Society na kulipa jina Tanzania Loans Society, Rais Kikwete alitia saini ya makubaliano ya wazi nchini marekani na zilitolewa fedha za mtaji wa kuanzishwa kwa tawi hili na jumuia ya madola nchini marekani kiasi cha shilingi billion miatano.

Lakini kutokana na majukumu ya Rais jakaya mrisho kikwete kuwa mengi hivyo ikawa ni vigumu kwa yeye kusimamia na kuendesha mradi huu hivyo aliamua kugawa majukumu haya kwa Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo na Ridhiwani Kikwete ambae ni mtoto wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Bank kuu ya Tanzania (B.O.T) na NMB.

Tanzania Loans Society inawakilishwa na Rais Jakaya kikwete, inaongozwa na General Manager Mh. Mizengo Pinda na inamilikiwa na Loan Officer Ridhiwani Kikwete kwa udhamini wa Rais Barack Obama. Lengo la kuanzishwa Tanzania Loans Society ni kutaka kuwasaidia watanzania wenye hali ya chini kimaisha

Nifursa kwa kila mtanzania mwenye umri wa miaka kuanzia 18 na mwenye akili timamu ajiunge na chama cha Tanzania Loans Society ili aweze kupata msaada wa kifedha.
Tutahakikisha kila mtanzania atakaejiunga na chama hiki kwa kujaza fomu ya uanachama na akachangia ada ya uanachama Tshs. 15,000 akawa mwanachama wa Tanzania Loans Society atapatiwa mkopo wa fedha anaohitaji pia kila atakaejiunga tutampatia zawadi ya uanachama / kianzio cha maisha Tshs.300,000 laki tatu bure.

Mtu yoyote anaruhusiwa kujiunga na mradi huu ili kutimiza ndoto zake unachotakiwa nikua na vigezo vifuatavyo, uwe ni mtanzania, uwe na akili timamu, uwe umetimiza miaka18 na uwe na kitambulisho cha aina yoyote ile. Kama unavigezo tajwa hapo unaruhusiwa kujaza fomu na ukajiunga ukawa mwanachama na kuchukua mkopo wa fedha kiasi chochote unachohitaji kuanzia laki moja na kuendelea, kila atakaejiunga nakua mwanachama wetu tutampatia zawadi ya shilingi laki tatu bure.


UTARATIBU WA KUJIUNGA:
Kujiunga na ili uwe mwanachama ni Rahisi Sana unachotakiwa ni kujaza fomu iliyopo Online katika tovuti hii utaiona Link hapo chini ya kujaza fomu imeandikwa "JAZA FOMU HAPA" katika fomu hii kuna sehemu utajaza kiasi cha fedha unachotaka ukopeshwe Ukishajaza fomu yote utatakiwa kuchangia mfuko wa wanachama kwa kulipia ada kama udhamini wako wa uanachama kiasi cha Tshs. 15,000 (elfu kumi na tano) baada ya kujaza fomu na kulipia ada ya Uanachama elfu kumi na tano kwa njia ya Tigopesa na M-Pesa katika namba ya M-Pesa pesa itapokelewa na muweka hadhina mkuu wa Tanzania Loans Society ambae pia ni muweka hadhina wa bank kuu ya Tanzania BOT namba yake ya kulipia kwa wateja wa Vodacom M-Pesa ni 0756 761 527 pia kwa wateja wa Tigo wanaweza kulipia katika namba ya muweka hadhina msaidizi wa Tanzania Loans Society kupitia Tigopesa namba 0656 736 416. ukishalipia utatumiwa Code namba yako ya Uanachama na ndani ya dakika30 utatumiwa kiasi cha fedha za mkopo uliohitaji na utatumiwa Tshs.300,000 laki tatu bure kama zawadi kwa kila mwanachama atakae jiunga.


MAREJESHO YA MKOPO:

Marejesho ya mkopo yataanza kufanyika baada ya miezi miwili kupita kuanzia siku uliyochukua mkopo, utakapopatiwa mkopo utatakiwa ukae miezi miwili bila kulipia na baada ya hapo utaanza kua unalipia kila mwezi Tshs. 60,000 (elfu stini) mpaka deni lako lote litakapokwisha na hakuna riba kwa sheria ya dini hivyo utakachokopa ndicho utakacholipa.


KWANINI UNAJIUNGA ONLINE NA UNALIPIA ADA TSHS.15,000 (ELFU KUMI NA TANO) TIGO PESA?

Hili swali ni muhimu na wengi wanajiuliza wengine wanaingiwa na hofu kuona fomu zinapatikana Online na kwanini mtu asije ofisini na kujiunga ofisini? Jibu nikwamba tumefanya hivi kurahisisha upatikanaji wa huduma hii kwa kila mtanzania kwani ofisi zetu zipo Dar es salaam makao makuu jirani na chuo cha IFM jengo la Utumishi wa Umma ghorofa namba 30 floor ya 5. Tumeweka utaratibu huu watu wajiunge Online ili kila mtanzania apate mkopo kwani sio wote wanaoishi dar es salaam kuna wengine wanaish mikoani hivyo tungesema wote waje ofisini kuna wengine watashindwa kufika katika ofisi zetu ndio sababu ya kuwataka watu wajiunge Online.

JINSI YA KUJIUNGA UPATE MKOPO:

Kujiunga ni rahisi sana bofya katika hiyo link ifuatayo hapo chini imeandikwa "JAZA FOMU HAPA" Utaikuta fomu ya kujiunga ijaze.


5636957_5c51f13a49.jpg
5636954_2c52085195.jpg

Ada ya Uanachama pamoja na Marejesho ya Mkopo vitalipiwa kwa njia ya Technologia ya Mobile banking kwa udhamini mkuu wa mitandao ya simu za mkononi Tigo na VodaCom ili kurahisisha huduma hii. Kwa wateja wa Tigo watalipia kupitia tigo pesa namba: 0656 736 416 au M-PESA 0756 761 527

MAREJESHO YA MIKOPO:
Kila atakaepatiwa mkopo atatakiwa akae miezi miwili (wiki8) kisha baada ya hapo atatakiwa kuanza kufanya marejesho kila mwezi kwa kulipia kiasi cha Tshs. 60,000 (elfu stini) kila mwezi mpaka deni lake litakapokwisha



Powered by Tanzanian Government Co-oparation (c)2012 sponsored by Obama Downs Association (ODA U.S.A Company)
ga.gif
 
Mungu wangu, hii ni DECI nyingine. Tafadhali wananchi wapewe hadhari wasiingie mkenge. Hapo kwenye weusi ndipo panapostahili mwelevu kujshituka. " Ada ya Uanachama pamoja na Marejesho ya Mkopo vitalipiwa kwa njia ya Technologia ya Mobile banking kwa udhamini mkuu wa mitandao ya simu za mkononi Tigo na VodaCom ili kurahisisha huduma hii. Kwa wateja wa Tigo watalipia kupitia tigo pesa namba: 0656 736 416 au M-PESA 0756 761 527

MAREJESHO YA MIKOPO:
Kila atakaepatiwa mkopo atatakiwa akae miezi miwili (wiki8) kisha baada ya hapo atatakiwa kuanza kufanya marejesho kila mwezi kwa kulipia kiasi cha Tshs. 60,000 (elfu stini) kila mwezi mpaka deni lake litakapokwisha
 
Hii inatofauti na yale 'mabilioni ya JK?'
Ule mpango wa awali(wa mabilioni ya JK) ulifanikiwa?
 
mtoto wa Riz alitolea ufafanuzi kuwa hakuna kitu kinachoitwa tanzania loan society. NI UTAPELI KUWA MAKNI RAIS HAUSIKI WALA PM.
 
Ukifuatlia hiyo namba ya voda inasema ni ya Zainabu Mrisho.Sasa hapa nimeshindwa kujua kama mwenye namna hiyo ni mtoto wa Kikwete au la maana mimi siwajui watoto wake wote kwa kweli.Kuna utapeli unanyemelea hapo.
 
mtoto wa Riz alitolea ufafanuzi kuwa hakuna kitu kinachoitwa tanzania loan society. NI UTAPELI KUWA MAKNI RAIS HAUSIKI WALA PM.

Asante kwa ufafanuzi kama amelisemea hilo.Kuna watu walitaka kuingia mkenge muda si mrefu
 
Kama hawahusiki kwa nini wasiwachukulie hatua wahusika kwa kutumia jina la kiongozi mkuu wa nchi kujipatia pesa kinyume cha sheria.... Hivi Nyerere angefanyiwa upuuzi kama huu???
 
lilishatolewa maelezo mkuu na mtoto wake kuwa huo ni utapeli so kwa wale waliotoa pesa waliliwa hela zao hakuna kitu kama hicho(ki nigeria zaidi)
 
Na Kama wavelength watu masikini kweli huo mikopo hauwafai na hauwezi kuwafikia Kamwe.ninaamini hakuna mkopo wala mchupa hapo huo ni wizi wa kwenye mtandao.
 
Robbery in the Information Age, you don't need to use much enegy, kiulaiiiiini, watu wanajiingiza.

"Powered by Tanzanian Government CO-OPERATION!!!"
NDO KITU GANI HIKI??????????
 
mmiliki wa namb hiyo tajwa hapo juu ya tigo anaitwa MICHAEL John. Sasa mpaka hapo mulika mwizi men.Ila kwa mtazamo wangu hii pia ni kashfa kwa vyombo vya dola haiwezeka jina la raisi wa nchi litumike kwenye mambo ya kishenzi nanmna hii labda kama swala hilo ni kweli ok ni mpango mzuri.
 
Mimi nimeanza kushtuka baada ya kuona eti Prime minister ndo anakuwa General Manager.
Hata kama ni utapeli huu sasa umekuwa aina yake.
Tatizo la Watanzania wengi wanapenda utajiri wa haraka ambao ni pamoja na kutaka vitu vya bure bure tu. ebu tujifunze kufanya kazi kwa bidii na tujiwekee malengo lakini pia tuwe wavumilivu ktk kusubiri malengo hayo kufikiwa
 
Daaa;bora nimepitia huku nilitaka jaza form mie mana naskia nchi IMEUZWA SO wajanja ndo watalipwa kwa style hii;kumbe majambazi aseee
 
Mungu wangu, hii ni DECI nyingine. Tafadhali wananchi wapewe hadhari wasiingie mkenge. Hapo kwenye weusi ndipo panapostahili mwelevu kujshituka. " Ada ya Uanachama pamoja na Marejesho ya Mkopo vitalipiwa kwa njia ya Technologia ya Mobile banking kwa udhamini mkuu wa mitandao ya simu za mkononi Tigo na VodaCom ili kurahisisha huduma hii. Kwa wateja wa Tigo watalipia kupitia tigo pesa namba: 0656 736 416 au M-PESA 0756 761 527

MAREJESHO YA MIKOPO:
Kila atakaepatiwa mkopo atatakiwa akae miezi miwili (wiki8) kisha baada ya hapo atatakiwa kuanza kufanya marejesho kila mwezi kwa kulipia kiasi cha Tshs. 60,000 (elfu stini) kila mwezi mpaka deni lake litakapokwisha

Jamani hivi mtaendelea kuwa watu wa kudanganywa kirahisi hivi na matapeli mpaka lini? Hivi hamuoni hata kiswahili kibovu kilichotumika kwenye hilo Tangazo au mnafanya makusudi? Hao sio kama Deci, hao ni matapeli wa bei rahisi wasio na fani yoyote ambao wanajaribu kuwapata watu wenye akili ndogo sana kama wao. Profile, history na details za hilo shirka hazieleweki na wala hawaeleweki. Msipoteze muda, mkituma hizo 15000 ndicho wanachokitaka na wala si kujenga mahusiano yoyote ya kibiashara na mtu yeyote. Majukumu ya rais na waziri mkuu huwa hayahusishi mambo kama hayo.
 
Back
Top Bottom