Rais Kikwete atengua uteuzi wa DC wa Kishapu


Yaah kwenye Cv yangu nimesema kuwa kuwa ni mpentecosti si unajua hii ina nguvu kuliko hata kusema kuwa ni mlokole? Na vyeo napanda sana na boss sijui hata kama anaamini kuwa mungu yupo! ( kwa lugha ya biblia ni Mpumbavu). Ila issue hii ni serius naweza kuwa sijaielezea vizuri sasa ila nikitulia nitaelezea vizuri. Ni mchanganiko wa mambo mengi kwenye hii issue ya huyu jamaa yes! ikiwemo kuwa jina lake ndiyo lilimpa ujaji na yeye anajua hivyo!
 
Shalom!!!

Ni hakika yangu kuwa watanzania sasa tunaingia kwenye kipindi kingine baada ya kile cha mwalimu ambaye pamoja hakuwa mtakatifu kama vile anavyotangazwa leo hii na wakatoliki lakini alikuwa na hofu kiasi fulani ya Mungu iliyomfanya akemee mambo mengi ambayo yangeleta ubaguzi. Ninasikitishwa sana na habari hiyo hapo juu kama kweli sasa inabidi ujulikane wewe nani kabla ya kupewa wadhifa. Watu wamchao Mungu inabidi Muombe kwa bidii hili lisiendelee. Kuna hoja pia Nimeona Waislamu wanalaumu kutotendewa haki unapoona hili basi ujue system imekaa vibaya kuna jinsi muheshimiwa anashindwa kubalance utendaji wake na taifa letu baba wa Taifa alishasema halina dini wala kabila.
Mungu awabariki sana. NA TUENDELEE KULIOMBEA TAIFA LETU
 
kwanini hakupewa kitabu cha imani yake toka mwanzo?
Na je kama han adini yoyote ingekuwaje?

Ina maana kuwa alipewa ujaji kwa upendeleo wa dini yake. Yaani jamaa walifikiri kuwa ni mwislamu mwenzao, kumbe siyo. Upo hapo WoS
 


Tafadhali nchi hii ina Dini ( kuna wakristo, waislamu na dini nyingine) kama nyerere alisema hivyo ndiyo laana hiyo inayotutokea. Huwezi kusema taifa haina dini maana yake nini? labda angesema kuwa kuwa serilai haipendelei dini yoyote lakini kusema nchi haina dini na sisi kukubali ulikuwa ni upumbavu ni sawa na kusema nchi haina mungu

Angalia nchi zilizojitia kimbelele kusema hazina dini, China ya wakati ule! (sasa Walokole kibao) Urusi (watajiju) North Korea (wanakula mpaka majani) wenzao south walishtukia sasa wako dunia ya kwanza na of course Tanzania mnajionea wenyewe
 
Inaposemwa Nchi haina dini maana yake ni kwamba serikali haiendeshwi kwa misingi ya IMANI fulani bali kwa mujibu wa taratibu ziliziwekwa na usawa kisheria.
Ila SISI tuna dini zetu sana tu. Ni vibaya na hatari sana kwa kiongozi yeyote anayechanganya dini au ukabila ktk utaalam wake wa kuongoza nchi.
Natamani bunge litunge sheria/ penal code ya Dini na Ukabila maana hivi vitu vimekatazwa ila havina adhabu yake endapo vitakiukwa.
 

Nyerere (RIP) kama mkristu mkatoliki hakumaanisha hayo unayotaka kutuambia. Alifafanua kuwa serikali haina dini rasmi katika kuongoza na kufanya maamuzi ya nchi. Zipo nchi kama Belgium (Roman Catholics), UK (Anglican), etc ambazo kuna dini rasmi katika kuongoza na kila kiongozi wake lazima awe wa dini hiyo (non-negotiable).

Lakini, turudi kwenye mada: Uteuzi wa wakuu wa wilaya haufanywi au haufanyiki kwa umakini. Wengi wanapewa kama zawadi na hii ndiyo staili ya muungwana. Nakumbuka alimteua Tom Mwang'onda kuwa mbunge kama zawadi ya kusaidiwa na fisadi mzee Mwang'onda. Listi ya vyeo zawadi ni kubwa tu (huo ni mfano tu)
 
Kwa hili, nani hasa alipaswa kuwa makini zaidi ya mwenzake? Rais au washauri wake au Usalama wa taifa?
 

Hii inanikumbusha stori moja miaka kama 10 iliyopita pale UDSM idara ya Hisabati. Kuna jamaa mmoja kwa kizanaki amekaa kihaya kabisa. Mama mmoja aliyekuwa mkuu wa idara hiyo alimsimamia kidete akitoa sababu kadha wa kadha ili aajiriwe maana alikuwa na GPA ndogo kuliko inayotakiwa (below 3.8) akijua fika kuwa ni mhaya mwenzake huku wakiachwa vijana wengine waliokuwa na GPA kubwa zaidi. Baada ya siku kadhaa jamaa kishaajiriwa, mama anamwuliza yule kijana "hivi wewe kule Bukoba umetoka sehemu gani"? Jamaa kasema mimi si wa Bukoba bali natokea Musoma. Mama aliishiwa nguvu na hana cha kufanya tena.
 

Jamani msisahau mwalimu Nyerere aliwahi kutamka kuwa ni hatari sana kuwa na kiongozi ambaye akiamuka asubuhi mkewe anamwambia chagua huyu,au simtaki huyu naye anakurupuka.Haya mambo yameanza pindi tu nchi ilipokosa viongozi.Leo hii inashangaza kusikia mtu kateuliwa na mara kuna matatizo je upekuzi Vetting ambayo mara zote hufanyika kabla ya uteuzi siku hizi wahusika wamelala au hata kiongozi wao naye alipachikwa tu bila upembuzi wa dhabiti.
 

Hayo aliyafanya Mwinyi wakati alipomteua Harun Mahundi akidhani ni maalimu
alimwambia kwamba tafadhali wakumbuke waislamu katika kutoa madaraka.
kwa hiyo issue ya udini nayo inachangia katika maswala yote haya.
 

Mamlaka ya uteuzi haiko serious kwani ilitakiwa kujiridhisha kwanza kabla ya kuteua mtu.
Awamu hii ya nne kuna culture ya mtu kuteuliwa kwa ushkaji (sio uwezo) ndio maana hata Usalama wa taifa wanashindwa kumchunguza anayeteuliwa kwani presumably ni 'mshkaji' wa MKUU.

Nchi hii tumekwisha!
 
mnashangaa hayo! bado tutaona mengi, hata kwa vile ataendelea kuteua washikaji msije kushangaa akamteua tena EL kuwa nanihiiiii.....!
 
Hii nchi Najuuuuuuuuta kuwa raia wake! Maana yanayofanyika utadhani hakuna Sirikali
 
Kweli kabisa hii inatokana na kuteua sana washikaji, siku moja tutaongozwa ata na ms............
 
Hii nchi kweli usanii umezidi ,ina maana wakati anamteua alikuwa hana taarifa/rekodi zake

I didn't expect an ignorantly operating government like this one. Tangu wilayani hadi taifa tuna maafisa usalama. kwa nini hawatumiki?

Au ndo matokeo ya kuedekeza urafiki na u-mtandao kuliko vyombo vya utendaji wa nchi.
 
Ameonewa tu. Viongozi wangapi wanakashfa tena nzito nzito. Kaonewa tu vile hana wa kumkinga.
 

Toka Oktoba 2007, Choya aliposhinda kesi mahakama kuu Bukoba, na ubunge wa marehemu Kabuye kutenguliwa, ni nani amekuwa mbunge wa Biharamulo Magharibi?

Li-website la bunge lilikuwa halijawa updated toka Oktoba 2007, mpaka Kabuye amekufa ndio wameshtuka, na leo wameondoa li-publication lililokuwa linasema Kabuye ni Mbunge wa Biharamulo West, as of yesterday. Well, Kabuye angekuwa mbunge asingefia njiani akielekea Dar kwenye mkutano wa TLP, angekuwa Dodoma bungeni.

Choya nae sijui hawakumpa barua rasmi kwamba wakuu wameghairi uteuzi? Maana kabeba familia kuapishwa kumbe kuna njemba nyingine iko gado. Anasema yuko njiani kwenda Dar kuuliza kwa nini wamem-fire maskini.
 

Heheheheheheeee....
 
Kweli kabisa hii inatokana na kuteua sana washikaji, siku moja tutaongozwa ata na ms............
unabahati invisible hajakuona...
ila nilishasema awali kwamba utashi wa kisiasa ndio unaangamiza nchi.
nadhani ethics zianze na watunga ethics wenyewe ndipo tuzidake huku. Haiwezekani nchi yenye vyombo vya kiutawala iignore ushauri au hata kuvishirikisha ktk maamuzi yenye maslahi ya taifa??
Nahitaji tuwe na adabu ktk hili pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…