Pamoja na kelele nyingi, lakini ikumbukwe kuwa, ni hisani ya CCM kwa kupitia matakwa ya wananchi katika kuendana na muda unaokuja mbeleni ndiyo iliona haja ya kuridhia mchakato wa kuwepo katiba nyingine ambayo itakidhi matakwa ya kitaifa kwa kipindi kingine kama cha maisha ya katiba hii ya mwaka 1977 tunayoitumia kwa sasa.
Kuna watu wanakuja na hoja za kusema Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 haikuainisha umuhimu wa kuwepo kwa katiba mpya lakini hao hao wanasahau kuwa ndiyo wananchi hao hao walioipatia CCM ridhaa za kuongoza nchi kwa mamilioni ya kura pamoja na kutokuwepo kwa kipengele cha mchakato wa kupata katiba mpya. Wananchi waliona ni CCM pekee itakayoweza kuwatengenezea mazingira mazuri katika upatikanaji wa katiba mpya ndiyo maana wakaamua kwanza kuipa kura za ushindi 2010 ili baada kwa kupitia CCM waweze kufikia malengo yao ya upatikanaji wa katiba mpya.
CCM haipo madarakani by default, la hasha bali imeendelea kuwepo kwa sababu kuu moja ambayo ni kuwaelewa wananchi walio wengi na kukubaliana na matakwa yao katika njia ya kuyafikia malengo yao bila kuwabagua hata wale wachache wenye malengo tofauti katika sera na Ilani za uchaguzi.
CCM ni amani, CCM ni upendo, CCM ni Mshikamano na CCM ni furaha.
CCM ni Itikadi, CCM ni sera, CCM ni Ilani ya uchaguzi na CCM ni ushindi.
Baada ya uchaguzi mkuu 2010, wananchi waliona kuna umuhimu wa kuandika katiba mpya na kwa sababu CCM ni chama kinachosikiliza mawazo ya wananchi wote (chama sikivu), basi kikaona kuna umuhimu wa kukubaliana na matakwa ya wananchi.
Wananchi wanafahamu kuwa, haiwezekani mwizi akaanza kukueleza njia ya kulinda nyumba yako wakati maisha yake yanategemea wizi, hii ina maana kuwa, haiwezekani wananchi wakakupa kura kwa kujipambanua tu wewe ni mwanademokrasia na kioo katika maendeleo ya taifa wakati ndani ya chama chako hakuna hata uhuru wa kutofautiana kimtazamo achilia mbali kifikra. Lakini kikubwa zaid, ubaguzi ndiyo kigezo cha utendaji ndani ya chama. Kama wewe hukubahatika kuzaliwa eneo lileee au hutoki kuleeee basi uwepo wako ndani ya chama unakuwa una mashaka makubwa labda uwe ni kondoo katika maamuzi yao ndani ya chama.